
Wakati mazungumzo kati ya serikali ya Kongo na AFC/M23 yakiendelea mjini Doha, hali ya bado ni ya wasiwasi. Katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Kivu Kusini, mvutano unaonekana, hasa pale Wazalendo – wapiganaji wanaoshirikiana na FARDC – wanafanya uvamizi na kushambulia maeneo ambayo hadi sasa yalikuwa chini ya udhibiti wa AFC/M23.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Siku ya Jumatatu, Aprili 14, milio ya risasi ilisikika katika sekta ya kaskazini ya Katana, iliyoko katika eneo la Kabare, kusini mwa Ziwa Kivu.
Mapigano haya yaliyoanza mwishoni mwa juma lililopita, yalizidi wiki hii, hususan katika eneo la Irhambi Katana, eneo ambalo ni makazi ya vituo viwili vya kibiashara katika eneo hilo, ambavyo ni Katana-centre, kusini na Kabamba, kaskazini, maeneo yanayotenganishwa kwa takriban kilomita kumi. Maeneo haya mawili yameathiriwa vibaya na mapigano.
Tangu saa 10 alfajiri ya siku ya Jumatatu, Aprili 14, milio ya risasi imesikika katika sekta ya kaskazini ya Katana, iliyoko katika eneo la Kabare, kusini mwa Ziwa Kivu. Kulingana na vyanzo vya ndani, mapigano hayo yalichochewa na shambulio la kuvizia la Wazalendo dhidi ya wapiganaji wa AFC/M23.
Mapigano hayo yalijiri katikati mwa Kabamba na mji jirani wa Mabingu, ulioko chini ya kilomita mbili kaskazini mwa Katana, takriban kilomita 10 kutoka hapo.
Wakiwa wamejihami hasa wakiwa na bunduki aina ya AK-47 na wakati mwingine wakiwa wamevalia sare za jeshi la FARDC, Wazalendo hawa, wenye asili ya Haut Plateau ya Kalehe, wao pekee yao ndio wanapigana na kuongoza mapigano dhidi ya AFC/M23.
Kutokana na makali ya mapigano, wakazi wa Kabamba walikimbia, wakiliacha soko kubwa zaidi katika mji huo ambalo hufanyika kila Jumatatu na Ijumaa. Mwisho wa siku, hali ya utulivu ilionekana kurejea katika eneo hilo.
Wapiganaji wa AFC/M23 wameanza kutwaa tena ngome walizopoteza katika siku za hivi majuzi.
Mapema jioni, vikosi vya AFC/M23 vilipeleka askari wao kwenye Barabara ya taifa Na. 2, kati ya Kavumba na Katana, vikiimarisha uwepo wao kwenye sehemu hii hadi Kabamba.