Sudani: Watu 400,000 walilazimika kukimbia kambi ya Zamzam Darfur

Takriban watu 400,000 walilazimika kukimbia kambi kubwa zaidi ya wakimbizi katika jimbo la Darfur nchini Sudani baada ya Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) kuchukua udhibiti, Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) limesema siku ya Jumatatu.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

“Kaya kati ya watu 60,000 na 80,000 walifurushwa kutoka kambi ya Zamzam [wakimbizi wa ndani] kutokana na kukithiri kwa ukosefu wa usalama,” IOM imesema katika taarifa yake.

Shambulio la RSF kwenye kambi hiyo lilisababisha mamia ya watu kupoteza maisha au kujeruhiwa, serikali na mashirika ya misaada wamesema.

Kundi la wanamgambo limeongeza mashambulizi katika eneo la magharibi la Darfur wakati likijaribu kuchukua mji mkuu wa mwisho wa jimbo hilo, el-Fasher, ambao bado hauko chini ya udhibiti wake.

Umoja wa Mataifa umesema siku ya Jumatatu kuwa zaidi ya watu 300, wakiwemo wafanyakazi 10 wa misaada ya kibinadamu, wameuawa katika mapigano ya Ijumaa na Jumamosi karibu na kambi za Zamzam na Abu Shouk karibu na El-Fashir.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *