Jumuiya ya nchi ya Kusini mwa Afrika SADC, imekanusha madai ya waasi wa M 23 kuwa kikosi chake cha SAMIDRC mwishoni mwa wiki iliyopita, wakishirikiana na jeshi la FARDC na wapiganaji wa Wazalendo, kilishiriki kwenye mapigano jijini Goma.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
SADC kwenye taarifa yake imesema, kikosi chake ambacho kipo kwenye mchakato wa kuondoka Mashariki mwa DRC, hakikushiriki kwenye operesheni ya pamoja, na kikosi cha DRC na makundi mengine ya wapiganaji yanayounga mkono wanajeshi wa serikali.
Aidha, SADC imesema inaheshimu mkataba ulioitwa saini kati ya kikosi chake na M23 tarehe 28 mwezi Machi kuhusu namna ya kuondoka Goma na inaunga mkono maamizio ya wakuu wa nchi za kikanda kuwa, suluhu ya mashariki mwa DRC ipatikane kwa njia ya mazungumzo.

Hali ya utulivu imerejea Goma, baada ya mapigano mazito usiku wa Ijumaa iliyopita, huku jeshi la serikali likiwashtumu M23 kwa kupotosha umma kuhusu makabiliano yaliyoshuhudiwa.
Watu 52 wameripotiwa kuuawa baada ya mapigano hayo kati ya Aprili 11 hadi 12, jijini Goma linalodhibitiwa na waasi wa M 23.
Wakati hayo yakijiri, mapambano makali yamezuka kati ya M23 na wapiganaji wa Mai-mai wakishirikianana Wazalendo katika baadhi ya vijiji vya wilaya ya Kabare na Mwenga huko Kivu Kusini.