Mpango wa Nyuklia w Iran: Mazungumzo yanaendelea katika pande zote

Kufuatia mazungumzo ya awali kati ya Marekani na Iran siku ya Jumamosi, Aprili 12, majadiliano kati ya nchi hizo mbili yanatarajiwa kuendelea mjini Roma wiki moja baadaye. Mkutano huu utatanguliwa na ziara ya mkuu wa shirika la Kimataifa la Nishati la Atomiki, Rafael Grossi, nchini Iran Jumatano, Aprili 16.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Jumamosi, Aprili 12, Marekani ilipongeza mazungumzo “chanya sana na yenye kujenga” kufuatia mazungumzo ya nyuklia ya Iran nchini Oman. Mazungumzo haya sasa yanapaswa kuendelea huko Roma mnamo Aprili 19.

Shirika la habari la serikali ya Iran, IRNA, pia limetangaza kwamba Mkuu wa Wakala wshirika la Kimataifa la Nishati la Atomiki (IAEA), Rafael Grossi, atazuru nchi hiyo siku ya Jumatano, Aprili 16. “Ni muhimu kuendelea na ahadi na ushirikiano na Shirika hilo wakati ambapo suluhu za kidiplomasia zinahitajika haraka,” ameandika kwenye mtandao wa X. Ziara yake ya awali nchini Iran ilikuwa mwezi Novemba. Kisha alitembelea maeneo ya nyuklia ya Natanz na Fordo.

Kabla ya duru mpya ya mazungumzo mjini Rome siku ya Jumamosi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi anatazamiwa kusafiri kwenda Moscow kujadili mazungumzo haya na Marekani, Tehran imesema. “Ningependa kueleza kwamba hii ni ziara ambayo tayari ilikuwa imepangwa,” amesema msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Esmail Baghai, akiongeza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwamba ziara hii “mwishoni mwa juma” itakuwa “fursa ya kujadili maendeleo ya hivi karibuni kuhusiana na mazungumzo.”

Makubaliano ya nyuklia

Urusi ni miongoni mwa nchi zilizotia saini makubaliano ya kimataifa ya nyuklia yaliyohitimishwa na Iran mwaka 2015, lakini ambayo sasa yamefutika tangu Marekani ilipoamua kujiondoa katika mkataba huo mwaka wa 2018. Makubaliano hayo yalitoa nafasi ya kuondolewa kwa baadhi ya vikwazo vya kimataifa dhidi ya Iran badala ya usimamizi wa mpango wake wa nyuklia na shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA). Kulingana na IAEA, Iran ilikuwa inaheshimu ahadi zake.

Lakini mnamo 2018, Donald Trump kwa upande mmoja aliondoa nchi yake kwenye makubaliano hayo na kurudisha vikwazo. Katika kulipiza kisasi, Iran tangu wakati huo imebadilisha ahadi zake hatua kwa hatua. Kwa hivyo, nchi imeongeza idadi na utendaji wa mitambo yake ya centrifuge, mashine zinazotumiwa kurutubisha uranium, ili kuzalisha zaidi, bora na kwa kasi katika vituo vyake vya Natanz na Fordo (katikati). Iran ndiyo nchi pekee isiyo na silaha za nyuklia iliyorutubisha uranium hadi kiwango cha juu (60%), huku ikiendelea kukusanya akiba kubwa ya nyenzo za nyuklia, kulingana na IAEA. Nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani kwa muda mrefu zimekuwa zikishuku kuwa Iran inataka kupata silaha za nyuklia. Tehran inakataa madai haya na inatetea haki ya nishati ya nyuklia kwa madhumuni ya kiraia, haswa kwa nishati.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *