
Rais wa China Xi Jinping anaanza ziara muhimu katikau kanda wa Asia ya Kusini-Mashariki kuanzia Jumatatu, Aprili 14, ambapo atazuru Vietnam, Malaysia na Cambodia. Ziara hiyo inalenga kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kidiplomasia huku kukiwa na mvutano wa kibiashara na Marekani.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Beijing, Clea Broadhurst
Rais wa China anaanza ziara yake nchini Vietnam, ambapo anatarajiwa kutia saini karibu mikataba arobaini ya ushirikiano katika nyanja muhimu: usafiri wa reli, kilimo, teknolojia ya kidijitali na maendeleo ya kijani. Lakini uhusiano unabaki kuwa mgumu, na hivi karibuni Vietnam iliweka ushuru wa kuzuia utupaji chuma kutoka China.
Kituo kinachofuata ni Malaysia. Ziara hii inawasilishwa kama hatua muhimu katika mahusiano baina ya nchi hizo mbili. Majadiliano hayo yanatarajiwa kulenga biashara na miundombinu. Cambodia, kwa upande wake, inasalia kuwa moja ya washirika wa karibu wa Beijing. Nchi imekamilisha hivi punde, kwa msaada wa China, uboreshaji wa msingi wa kimkakati wa jeshi la majini.
Asia ya Kusini-Mashariki, eneo muhimu la kiuchumi kwa Beijing
Asia ya Kusini-Mashariki ni eneo muhimu la kiuchumi kwa Beijing. Mnamo 2024, Jumuiya ya Nchi za Mataifa ya Kusini-Mashariki mwa Asia walikuwa wateja wakubwa wa mauzo ya nje ya China, wakiongozwa na Vietnam na Malaysia.
Xi Jinping pia anataka kusisitiza ushirikiano katika teknolojia zinazoibukia, kama vile 5G na AI, ili kuimarisha minyororo ya ugavi ya kikanda.
Kutokana na hali ya vita vya kibiashara na Marekani, Beijing inataka kujiweka kama mshirika thabiti mbele ya Marekani inayozidi kutotabirika, kwa kuzingatia ushirikiano wa kikanda, uvumbuzi wa kiteknolojia na ushirikiano wa kiuchumi.