
Rais anayemaliza muda wake nchini Ecuador, Daniel Noboa amechaguliwa tena Jumapili, Aprili 13, kwa karibu 56% ya kura baada ya siku isiyo hiyo kushuhudia rekodi ya watu kujitokeza kwa wingi katika uchaguzo huo. Karibu 84% ya wapiga kura milioni 13.7 wa Ecuadorwameshiriki uchaguzi huo. Matokeo ambayo mpinzani wake wa mrengo wa kushoto Luisa Gonzalez amesema hayatambui.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Nchini Ecuador, kulingana na matokeo ambayo bado ni ya muda yanayojumuisha 92% ya kura, Daniel Noboa anaongoza mbele ya Luisa Gonzalez kwa 56% dhidi ya 44%. Hali hii, kwa mujibu wa takwimu za Baraza la Taifa la Uchaguzi (CNE), imejitokeza haraka wakati wa kuhesabu kura.
“Ushindi huu ni wa kihistoria, ushindi kwa zaidi ya pointi 10, ushindi wa zaidi ya kura milioni moja ambao hautii shaka kwa mshindi,” Daniel Noboa, 37, amewaambia waandishi wa habari kutoka eneo la mapumziko la bahari la Olon magharibi mwa nchi, kwenye pwani ya Pasifiki.
Mpinzani wake, ambaye amemshinda kwa kura ndogo katika duru ya kwanza mnamo mwezi wa Februari (chini ya kura 17,000), amesema mapema kutoka mji wa Quito kwamba hatambui matokeo. “Ninakataa kuamini kuwa kuna watu wanaopendelea uwongo badala ya ukweli (…) tutadai hesabu mpya na kufunguliwa kwa masanduku ya kura,” ametangaza mrithi wa kiongozi wa zamani wa kisoshalisti Rafael Correa (2007-2017).
Kwa kweli kushindwa huku kwa pointi 11 ni mshangao kwa watu wengi nchini Ecuador baada ya duru ya kwanza ambapo Luisa González alishindwa na Rais Daniel Noboa kwa pointi ndogo tu, anabainisha mwanahabari wetu huko Quito, Eric Samson.
Luisa Gonzalez, wakili mwenye umri wa miaka 47, alitamani kuwa mwanamke wa kwanza kuongoza nchi. Alishindwa mnamo mwezi Oktoba 2023 na Daniel Noboa, ambaye alipigwa na mshangao katika uchaguzi ulioitishwa na mtangulizi wake Guillermo Lasso. Katika duru ya kwanza, baada ya matokeo haya ya kura zinazokaribiana, Daniel Noboa ndiye ambaye alishutumu “makosa mengi”, tuhuma zilizokataliwa na waangalizi wa kimataifa waliofuatilia uchaguzi huo.
Luisa Gonzalez, kwa upande wake, ameishutumu serikali kwa “vitendo vya kukatisha tamaa” vinavyolenga kubadili matokeo ya uchaguzi. Rais wa CNE Diana Atamaint alionya siku ya Jumapili asubuhi: “Lazima tukatae kwa uthabiti mazungumzo ya ulaghai; shutuma zisizo na uthibitisho sio tu zinadhuru taasisi hii, lakini pia zinadhoofisha imani katika demokrasia yenyewe.”
Kampeni chini ya mvutano Jarida
Mrithi wa mfanyabiashara mkubwa wa ndizi, Daniel Noboa anajumuisha wasomi wa kisiasa wa Ecuador kutoka ulimwengu wa biashara. Katika mitandao ya kijamii, anatumia vibaya sura yake kama kiongozi mchanga ambaye anashikilia msimamo mkali juu ya usalama, unaojulikana kwa kutuma askari mitaani na magerezani, sera iliyokemewa na mashirika ya haki za binadamu.
Luisa Gonzalez alipendekeza kuongezeka kwa matumizi katika miundombinu na huduma za umma katika nchi iliyo katika mdororo wa uchumi, iliyokumbwa na umaskini na kazi ngumu. Mwanasheria huyo, ambaye anajionyesha kama mwanamke rahisi, mama asiye na mwenzi aliyejitolea mwenyewe, pia aliahidi usalama, lakini heshima kubwa kwa haki za binadamu.