
Rais wa Togo Faure Gnassimbé ameteuliwa rasmi kuwa mpatanishi wa Umoja wa Afrika kutatua mzozo unaoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Anamrithi Rais wa Angola Joao Lourenço, ambaye alishikilia wadhifa huo hadi mwezi uliopita. Mamlaka ya Togo haikujibu maombi ya RFI ya kutoa maoni kuhusu uteuzi huu.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Robert Dussey, Waziri wa Mambo ya Nje wa Togo, amezishukuru nchi za Umoja wa Afrika “kwa imani iliyoonyeshwa kwa rais wa Togo.” Mpatanishi aliyeteuliwa kutatua mzozo unaoendelea mashariki mwa DRC, anahakikisha kwamba Faure Gnassimbé “atachangia kikamilifu katika kutafuta amani ya kudumu” katika eneo la Maziwa Makuu.
Lakini chaguo hili la rais wa Togo limezua utata: takriban mashirika kumi na tano ya Togo yameshutumu ukosefu wa uhalali kwa upande wa rais wao. Louis Rodolphe Attiogbé, wa vuguvugu la Novation Internationale, hafichi mashaka yake.
Tulishangazwa na uteuzi wake, mtu anayekiuka haki zote za raia katika nchi yake.
Kazi inaonekana ngumu kwa rais wa Togo. Mtangulizi wake, Rais wa Angola Joao Lourenço, alikumbana na vikwazo kadhaa vya kidiplomasia. Tangu mwishoni mwa mwaka 2021, nusu dazeni za makubaliano na usitishaji mapigano yametangazwa mashariki mwa DRC, ambayo yote yamevunjika haraka. Hatua ya kwanza kwa rais wa Togo itakuwa kuunganisha na kuoanisha michakato miwili iliyopo ya upatanishi: ile ya Luanda na Nairobi, ili kuepuka kuzidisha njia za majadiliano.
Hasa tangu kwa wiki kadhaa sasa, Qatar pia imekuwa ikifanya mchakato sambamba wakuwezesha kupayikana kwa amani mashariki mwa DRC huko Doha. Hapo ndipo mwishoni mwa mwezi Machi, kwa mshangao wa kila mtu, na baada ya majaribio kadhaa ya Umoja wa Afrika kushindwa, marais wa Rwanda na Kongo hatimaye walikubaliana kukutana.