
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International, limetuhumu serikali ya Ethiopia kwa kuwafurusha kwa nguvu raia wake katika makaazi yao ili kupisha mradi wa serikali wa kupanua baadhi ya miji na mitaa.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Katika ripoti yake Amnesty International, imesema mamlaka nchini Ethiopia zinatumia mabavu kuwafurusha raia katika maakazi yao, ikiwemo kukosa kutoa ilani ya kuhama kwa muda unaofaa na kukosa kutoa fidia kwa waathiriwa.
Shirika hilo la kimataifa limeongeza kuwa idadi kubwa ya raia kwa sasa wanaishi kwa hofu wakihofia kwamba pia wataathirika, tangu serikali waziri mkuu Abiy Ahmed kuanza mradi huo mwaka 2022
Haimanot Ashenafi ni mtafiti wa Amnesty International nchini Ethiopia.
“Kufurusha kwa waakazi hao kunakiuka sheria za kimataifa, na pia sheria za Ethiopia, pamoja na maadili ya kikanda ambayo Ethiopia ni mwanachama. Ilani ya kutosha sharti iwe kwa maandishi, lakini hapa wakaazi waliambiwa kuhama makwao kwa kauli ya mdomo tu. Cha msingi hapa ni kwamba hili ni swala la haki za binadamu maana linawafanya raia wengi kukosa makaazi, na kukiuka haki zao na linaweza athari maisha yao siku zote.” Alisema Haimanot Ashenafi, mtafiti wa Amnesty International nchini Ethiopia.
Amnesty International, sasa inataka serikali jamii ya kimataifa kuingia kati ili kuzuia serikali ya Ethiopia kuendelea kukiuka haki ya raia kuwa maakazi, hadi pale matwaka yote raia hasa kuhusu haki zao yatakapongatiwa na serikali.