Paris Marathon: Mkenya Bernard Biwott ashinda kwa mara ya pili mbio za marathon

Mkenya Bernard Biwott ameshinda mbio za Marathon (marathon) kwa mara yake ya pili siku ya Jumapili Aprili 13 mjini Paris, akimaliza kwa muda wa saa 2 dakika 5 na sekunde 25, akiboresha ubora wake binafsi, baada ya kuwaangusha washindani wake wote kilomita 10 kufikia hatua ya mwisho.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Akiwa na umri wa karibu miaka 23, mkimbiaji  huyo alikuwa akishiriki tu katika mashindao ya mbio ndefu kwa mara yake ya pili katika mashindano haya, baada ya yaleya Frankfurt mnamo Oktoba 2024, ambayo pia alishinda. 

Raia wa Djibouti Ibrahim Hassan, ambaye ndiye pekee aliyemfuata Mkenya huyo katika kuongeza kasi yake, alimaliza wa pili kwa saa 2 dakika 6 na sekunde 13, mbele ya Mkenya mwingine, Sila Kiptoo, ambaye alivunja rekodi yake binafsi kwa karibu dakika mbili (saa mbili dakika sita na sekunde 21).

Muethiopia Bedatu Hirpa amemshinda mwenzake Dera Dida katika hatua ya mwisho siku ya Jumapili, na kushinda kwa saa 2 dakika 20 sekunde 45. Akiwa na umri wa miaka 25, alishinda marathon yake ya pili ya mwaka, baada ya kushinda huko Dubai katikati ya mwezi wa Januari mwaka huu, akiongoza mbele ya Dida katika hatua ya kumaliza.

Baada ya kutoa nafasi katika mita za mwisho, Dera Dida alimaliza kwa saa 2 dakika 20 sekunde 49. Mwanariadha wa Kenya Angela Tanui alishika nafasi ya mwisho kwenye jukwaa akitumia muda wa kukimbia wa saa 2 dakika 21 na sekunde 7.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *