
Marekani na Iran zimeanza mazungumzo yasiyokuwa ya moja kwa moja, kuhusu mradi wa nyuklia, huku rais Donald Trump akitishia hatua ya kijeshi iwapo, mkataba hautapatikana.Iran inasema haitarajii mazungumzo hayo yatachukua muda mrefu.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Wajumbe kutoka mataifa hayo mawili, wameanza mashauriano jijini Muscat, Oman kupitia wawakilishi, baada ya Marekani kutaka mazungumzo ya ana kwa ana.
Hata hivyo, kuliibuka na tofauti kuhusu namna ya kushiriki kwenye mazungumzo hayo, yanayolenga kusaidia kupatikana kwa mkataba mpya, baada ya Trump kufuta mkataba wa awali, mwaka 2018.
Iran inawakilishwa na Waziri wake wa Mambo ya nje Abbas Araghchi, huku Marekani ikiwakilishwa na mjumbe maalum wa Trump, Steve Witkoff.
Ujumbe kutoka Iran unasema, unalenga kupata maelewano yatakayokuwa na manufaa kwa pande zote mbili, huku Marekani ikiendelea kuweka shinikizo kwa Iran.
Nchi ya Israel, mshirika wa karibu na wa kuaminiwa wa Marekani, imekuwa ikitaka Tehran kuzuiwa kutengeneza silaha za nyuklia, ambazo zinatishia usalama wake.