Hamas inasema Israel imeshambulia hospitali ya Al-Ahli Baptist Gaza

Kundi la wapiganaji wa Hamas limethibitisha kuharibiwa kwa chumba cha wagonjwa mahututi na kile cha upasuaji katatika shambulio la Israel dhidi ya hospitali kuu katika Ukanda wa Gaza.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na video iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii, moshi mkubwa umeonekana ukitoka katika hospitali ya Al-Ahli Baptist baada ya kombora kulenga jengo lenye orofa mbili.

Mkanda huo wa video pia umeonyesha namna ambavyo baadhi ya wagonjwa ambao walikuwa wamelazwa waliovyoondolewa kwa dharura kutoka kwenye jengo hilo.

Mwanahabari kutoka kwenye Ukanda wa Gaza amedai kwamba wanajeshi wa Israel walimpigia simu daktari katika hospitali hiyo wakimtaka kuwaagiza wagonjwa wote kuondoka kwenye jengo hilo kabla ya shambulio hilo.

Uharibifu uliotokana na shambulio la Israel dhidi ya hospitali katika Ukanda wa Gaza
Uharibifu uliotokana na shambulio la Israel dhidi ya hospitali katika Ukanda wa Gaza REUTERS – DAWOUD ABU ALKAS

Inaripotiwa kwamba wahudumu kwenye hospitali hiyo walitakiwa kuwaondoa watu wote kwa muda wa dakika 20 peke.

Hamas inasema inachunguza shambulio hilo ikiituhumu Israel kwa kutekeleza uhalifu mbaya.

Hadi tukichapisha ripoti hii idadi ya watu waliofariki katika shambulio hilo haikiwa imeekwa wazi.

Al-Ahli ndio hospitali pekee ambayo bado inafanya kazi katika Ukanda wa Gaza baada ya kuharibiwa kwa hospitali ya Al-Shifa kaskazini mwa eneo hilo.

Mnamo Oktoba 2023, shambulio katika hospitali hiyo hiyo liliua mamia ya watu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *