Kichuya azitaja mechi tano za moto bara

WINGA wa JKT Tanzania, Shiza Kichuya amesema katika mechi tano zilizosalia kumaliza msimu huu anaziona ni za jasho na damu kutokana na kila timu kuwa na hesabu kali na ugumu hazichagui uwanja wa nyumbani wala ugenini.

Kichuya kacheza mechi 17 kati ya mechi 25 iliyocheza timu hiyo ikiwa n dakika 1151 akifunga mabao mawili na asisti mbili, alitolea mfano mechi ya Aprili 10, iliyopigwa Uwanja wa Meja Generali ISamuhyo dhidi  Namungo iliyomalizika kwa sare ya mabao 2-2 namna ilivyokuwa ngumu hadi wakajikuta wanaambulia pointi moja, wakati malengo yao ilikuwa kuvuna alama tatu.

 “Ni kawaida ligi inapofika mwisho ugumu kuongezeka, hivyo kama wachezaji tunajitahidi kuongeza umakini kila mechi ili kuyafikia malengo yetu,” alisema Kichuya aliyewahi kung’ara akiwa na  Simba aliyoitumikia msimu wa 2017-2019 akaondoka kwenda kujiunga kwa mkopo na Klabu ya Enppi ya Misri kisha akarejea tena Msimbazi 2020.

Nyota huyo alisema kwa sasa hawezi kutanguliza maslahi  binafsi ila timu akitamani kumaliza nafasi angalau kuanzia ya sita: “Tuna kazi ngumu lakini tutaendelea kupambana kuhakikisha mechi zilizosalia zinakuwa za mafanikio kwetu.”

Winga huyo msimu uliyopita katika mechi 25 alifunga mabao matano, asisti moja,  dakika 1050, jambo linaloonyesha  Ligi Kuu inayoendelea ameshindwa kuyafikia mabao hayo huenda akafanya hivyo katika mechi tano zilizo salia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *