
Raia 11 wa Urusi waliokuwa wamezuiwa nchini Tunisia tangu mwezi Novemba kwa madai ya ugaidi, wameachiwa huru na hivi karibuni watarejeshwa nchini mwao.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Kuachiwa huru kwa raia hao wa Tunisia, kumethibitishwa na Shirika la Habari la Urusi.
Watu hao walikamatwa, katika mpaka wa Tunisia na Algeria, huku polisi wakiwatuhumu kumiliki mtambo waliopanga kutumia kwenye shughuli za kigaidi.
Raia hao wa Urusi, walikuwa wamekwenda nchini Tunisia kama watalii lakini wakajipata chini ya ulinzi kwa tuhma za ugaidi.
Hata hivyo, taarifa zaidi hazijafahamika kuhusu kuachiwa kwa raia hao wa kigeni, lakini taarifa kutoka ubalozi wa Urusi imesema, raia wake watarejea Moscow siku ya Ijumaa.
Tunisia ni nchi mojawapo inayovutia watalii wengi Kaskazini mwa Afrika ambayo hupendelewa na raia wengi wa Urusi.