Gabon: Uchaguzi wa urais kufanyika Aprili 12, kampeni za uchaguzi zafikia tamati

Kampeni za uchaguzi wa urais nchini Gabon zimemalizika siku ya Alhamisi na uchaguzi wa urais umepangwa kufanyika Jumamosi, Aprili 12, ambapo wagombea wanane wanawania kwenye kiti cha urais.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Ingawa kwa kawaida viongozi wa mpito hawaruhusiwi kugombea uchaguzi, Gabon iliidhinisha katiba mpya kwa kishindo mwezi Novemba iliyompa fursa Brice Oligui Nguema.

Mahakama ya Katiba ya Gabon iliidhinisha orodha ya wagombea wanane kugombea katika uchaguzi wa urais wa taifa hilo la Afrika ya Kati uliopangwa kufanyika Arili 12, akiwemo Rais wa mpito Brice Oligui Nguema, ambaye alichukua mamlaka katika mapinduzi ya kijeshi mwaka 2023.

Wagombea wengine walioidhinishwa na mahakama ni pamoja na Stephane Germain Iloko Boussengui, mwanachama wa zamani wa Chama cha Kidemokrasia cha Gabon ambaye ameunda vuguvugu lake, na mkaguzi wa ushuru Joseph Lapensee Essigone.

Mjasiriamali wa Gabon Gninga Chaning Zenaba ndiye mwanamke pekee anayewania katika uchaguzi huo.

Nguema mwenye miaka 50 aliumaliza utawala wa muda mrefu wa rais Ali Bongo na familia yake kwa mapinduzi. Mpinzani mkuu wa Nguema ni waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Alain Claude Billie By Nze ambaye anawania kwa tiketi ya mgombea binafsi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *