Beijing yaongeza ushuru wa bidhaa za Marekani hadi 125% na inatafuta washirika

China imetangaza siku ya Ijumaa Aprili 11 kwamba itaongeza tozo zake za forodha kwa bidhaa za Marekani hadi 125%, kuanzia kesho Jumamosi. Hili ni ongezeko jipya la vita vya kibiashara kati ya China na Marekani. Na Wizara ya Biashara, kwa upande wake, inatangaza kwamba malalamiko mapya yatawasilishwa kwa Shirika la Biashara Duniani (WTO).

Imechapishwa:

Dakika 3

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Alhamisi serikali ya Marekani ilitangaza kwamba ushuru wake kwa bidhaa za China sasa ulikuwa ni 145%, na hivyo kuondoa matumaini ya kupungua kwa vita vya kibiashara vilivyoanzishwa na Donald Trump. Baada ya hayo, China imetangaza siku ya Ijumaa kwamba itaongeza ushuru wa kulipiza kisasi kwa bidhaa za Marekani hadi 125%, saa chache baada ya Xi Jinping kutangaza kuwa “hakuna washindi katika vita vya ushuru.” Kulingana na Tume ya Ushuru wa Forodha ya China, viwango hivyo vipya vinatarajiwa kuanza kutumika siku ya Jumamosi.

“Ushuru wa juu” wa Marekani dhidi ya China “si chochote zaidi ya mchezo wa nambari usio na maana ya kiuchumi” na “umekuwa mchezo,” kulingana na Wizara ya Biashara ya China. Beijing inaonya kwamba hatua yoyote ambayo inadhuru maslahi yake itakabiliwa na mashambulizi, anaripoti mwandishi wetu wa Beijing, Cléa Broadhurst.

Washington huchochea machafuko

Serikali ya China inamtuhumu Donald Trump kwa kuchochea machafuko katika masoko na ushuru wake mkubwa ambao umetikisa uchumi wa dunia. China inasema Marekani lazima “ichukue jukumu kamili.” Inaonya kuwa haitakii kuendelea kujilinganisha na ongezeko linalofuata la ushuru wa forodha wa Marekani. Kwa mujibu wa Beijing, bidhaa kutoka Marekani zimekuwa hazifai katika soko la China kwa sababu ya ushuru uliyowekwa.

Na ujumbe uko wazi: ikiwa Washington itaendelea na njia hii, China haitajibu tena kwa utaratibu na hatua sawa. Haya ni mabadiliko ya mkakati katika msuguano wa kibiashara kati ya mamlaka hizo mbili.

Wizara ya Biashara, kwa upande wake, imetangaza kwamba malalamiko mapya yatawasilishwa kwa Shirika la Biashara Duniani. Kipindi kipya katika mgogoro wa kisheria na kiuchumi kati ya nchi hizi mbili zenye uchumi mkubwa duniani.

Kwa hiyo China inatafuta kuimarisha ushirikiano wake mwingine…

Kwa upande wa kidiplomasia, China inaongeza mawasiliano na washirika wake wakuu, hasa Umoja wa Ulaya na nchi za Kusini Mashariki mwa Asia. Chin imejibu, wakati Donald Trump amesitisha ushuru wa forodha kwa nchi kadhaa …

Rais Xi Jinping wa China amefanya mazungumzo na viongozi kadhaa wa Ulaya, akiwemo Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez, siku ya Ijumaa, ambaye alikuwa katika ziara yake ya tatu mjini Beijing. Lengo: kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kuonyesha umoja mbele ya sera za ulinzi za Marekani. Xi Jinping amesisitiza haja ya kupinga kile alichokiita “vitisho vya upande mmoja” na kutetea sheria za biashara ya kimataifa.

Xi Jinping pia anatarajiwa nchini Vietnam, Malaysia na Cambodia wiki ijayo. China inapolipiza kisasi dhidi ya ushuru wa forodha wa Marekani, nchi nyingine za Asia, zinazotegemea sana mauzo ya nje kwenda Marekani, zimejishusha mbele ya Marekani. Nchi hizi ni Vietnam na Cambodia, wazalishaji wa nguo na wanachama wa Jumuiya ya Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia (ASEAN), ambayo tayari imetangaza kwamba haitachukua hatua za kulipiza kisasi.

Hanoi inatarajia kupunguza kodi hizi kwa nusu, ambazo kwa sasa ni 46%. Hoja ya serikali ya Vietnam: imeahidi kupambana na wizi wa mali miliki na usafirishaji haramu. Bidhaa nyingi zinazotengenezwa nchini China kwa hakika hufika katika ardhi ya Vietnam, ambazo husafirishwa tena hadi nchini Marekani, lakini wakati huu chini ya lebo ya Made in Vietnam, zikinufaika na ushuru wa chini wa forodha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *