
Nchini Guinea, Wizara ya Ugatuaji (MATD) itaandaa uchaguzi wa mwisho wa mpito, na sio Tume Huru ya Uchaguzi ya Taifa (CENI) kama ilivyokuwa tangu mwaka 2010. Maafisa kadhaa wa mpito walikuwa tayari wametaja chaguo hili katika miezi ya hivi karibuni, na sasa ni rasmi. Kwa hivyo MATD itaandaa kura ya maoni ya katiba iliyopangwa kufanyika Septemba 21 na uchaguzi wa kuashiria mwisho wa mpito, uliotangazwa hadi mwisho wa mwaka 2025.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Conakry, Tangi Bihan
Uamuzi huu unapingwa na vyama kadhaa vya kisiasa, vinavyotaka kuanzishwa upya kwa CENI, inayochukuliwa kuwa haina upendeleo.
Tangazo hilo lilitolewa siku ya Jumatano hii, Aprili 9, nchini Guinea, wakati wa mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na Djenabou Touré, mkurugenzi wa kitaifa anayehusika na masuala ya kisiasa na usimamizi wa uchaguzi ndani ya Wizara ya Ugatuaji.
Aliongeza kuwa mamlaka itaanzisha “uangalizi” ambapo wawakilishi wa vyama vya siasa na mashirika ya kiraia wataweza “kufuatilia” na “kusimamia” matendo ya wizara. Kulingana na Djenabou Touré, uamuzi huu unafuatia mapendekezo ya “mazungumzo ya kisiasa kati ya wananchi wa Guinea” yaliyofanywa mwaka 2022, lakini yakisusiwa na vyama vikuu vya kisiasa nchini humo.
Mamlaka ya mpito haijawahi kufanya siri yoyote ya mashaka yao kuelekea CENI. Maafisa kadhaa walisema katika miezi ya hivi karibuni kwamba Tume Huru ya Uchaguzi (CENI) itasababisha gharama kubwa na i chanzo cha migogoro ya uchaguzi. Maafisa kutoka chama cha UFDG cha Cellou Dalein Diallo na chama cha UFR cha Sidya Touré, vyama vikuu viwili vya kisiasa nchini humo, vinachukulia uamuzi huu kuwa kinyume cha sheria na wanatoa wito wa kurejeshwa kwa CENI, ambayo inachukuliwa kuwa katika nafasi nzuri zaidi kuandaa uchaguzi huru na wa uwazi.
Dansa Kourouma, rais wa CNT, bunge la mpito, alibaini Aprili 10 kwamba rasimu ya awali ya katiba ilipitishwa wakati wa kikao cha faragha. Hakuna waandishi wa habari walioruhusiwa kuhudhuria mijadala hiyo. Rasimu hii ya awali ya Katiba, ambayo nakala yake haijawekwa wazi, sasa iko mikononi mwa rais wa mpito, Mamadi Doumbouya.