Kuendesha na kudumisha mifumo ya usimamizi wa maji salama hakuwezi kufanikiwa bila uwekezaji mpya na utaalamu wa kiufundi, hususan ukizingatia ongezeko la idadi ya watu katika maeneo ya mijini nchini Tanzania.
Matumizi ya mifumo ya mabomba kama vile ya Weholite HDPE yanatoa masuluhisho ya muda mrefu dhidi ya changamoto ya usimamizi wa maji ya mvua kubwa ambayo yanaonekana kuharibu maeneo mengi ya mijini, maeneo ya makazi yasiyopangwa vizuri na mtandao mpana wa uchukuzi nchini kote.
Mifumo ya mabomba makubwa ya Weholite HDPE yanayotengenezwa na Kampuni ya Megapipes Solutions Limited, katika kiwanda chao cha kisasa kilichopo Kigamboni, Dar es Salaam, kinatoa njia mbadala na endelevu za kutatua changamoto za mafuriko, maji taka (majumbani na viwandani) na uhifadhi wa maji nchini Tanzania, kulingana na wahandisi wanaotekeleza miradi ya miundombinu.

Mabomba ya DN1800 HDPE Weholite yenye uwazi kwa juu yaliyowekwa katika Mtaa wa Chato, Dar es Salaam.
Miundombinu ya Usafiri
Mitandao ya barabara na reli ya Tanzania inaendelea kupanuliwa kwa kasi, ikichangiwa na ukuaji wa uchumi na hitaji la mifumo bora ya usafiri, na hilo linafanya mabomba ya Weholite kuwa bora kwa ujenzi wa barabara kwa sababu yanastahimili kutu na mikwaruzo, ni rahisi pia kufungwa na yanadumu kwa zaidi ya miaka 100.
TANROADS na TARURA zinaendelea kuwa taasisi za kwanza kutumia teknolojia hii, kwa sababu uimara wa asili wa makalvati ya Weholite yameongeza ufanisi na hayana changamoto nyingi. Ujenzi wa barabara sio kwa ajili ya kupitisha vyombo vya moto pekee, bali unaleta ahueni kubwa kwa jamii kwa ujumla.
Mfano mzuri wa hivi karibuni ni katika kijiji cha Somanga, mkoani Lindi, ambapo barabara kuu muhimu inayounganisha Dar es Salaam, Lindi, na Mtwara iliathiriwa vibaya wakati mafuriko ya El Niño yaliyolisomba daraja mwezi Mei 2024. Daraja hili lilikuwa kiungo muhimu cha magari madogo na makubwa yaliyokuwa yakisafirisha mizigo barabarani, hivyo kurahisisha biashara na usafirishaji katika mkoa huo.
Kadhia hiyo ilileta athari kubwa za kiuchumi, ikizuia na kuchelewesha usafirishaji wa bidhaa kwa ajili ya biashara za ndani. Hata hivyo, kwa kurejelea ufungaji wa makalvati ya Weholite uliopita, TANROADS ilichagua kutumia makalvati ya Weholite yenye kipenyo cha DN2000 kujenga upya daraja hilo.
Uamuzi huu ulihakikisha kuwa daraja hilo linajengwa upya kwa haraka na ndani ya muda, na kupunguza usumbufu kwa jamii na kuruhusu shughuli za kiuchumi kuendelea kama kawaida.
Miundo iliyofukiwa chini ya uso wa barabara inahitaji kuwa na sifa za kipekee ili kuhimili mashinikizo ya kila wakati yanayotokana na msongamano mkubwa wa magari unaopita kwenye barabara iliyo juu. Mabomba ya Weholite yameundwa mahsusi kwa kuzingatia hili.
Makalvati hayahitaji kuzungushiwa zege, badala yake udongo unaofaa kwa ajili ya barabara una mwagwa kila upande wa bomba la Weholite na kushindiliwa. Kuta za pembeni (wing walls) na kuta za juu (head walls) hujengwa ili kuhakikisha udongo haumomonyoki, jambo ambalo litasaidia pia kuhakikisha kuwa barabara haiharibiki kunapotokea mafuriko.
Makalvati ya Weholite yanayodumu na yenye ufanisi katika kuhakikisha maji yanapitishwa ipasavyo ili yatiririke bila kukatizwa. Pia, ujenzi wa mihimili mepesi ya makalvati ya Weholite unarahisisha uwekaji wake, kuwezesha mtiririko wa maji bila kikwazo, na ni rafiki wa mazingira. Makalvati husafirishwa kwa urahisi bila kukatika tofauti na yale ya zege, huu ndiyo mustakabali wa ujenzi wa barabara.
Mifereji ya maji
Ukitembelea barabara za baadhi ya maeneo yenye watu wengi katika miji ya Tanzania zina kitu kimoja cha kufanana, ambacho ni mifereji ya maji iliyo wazi. Hii hupatikana zaidi katika maeneo ya mijini na hutumiwa kwa kumwaga maji ya mvua, hususan wakati wa mvua kubwa. Maji ya mvua yanayokusanywa na njia hizi mara nyingi huelekezwa kwenye mito au njia nyingine za maji.
Ujenzi wa mifumo ya mifereji ya maji wazi ni utamaduni ambao umedumishwa kwa miongo kadhaa. Dar es Salaam inakabiliwa na mafuriko, na pia ni sehemu ambayo inajulikana sana kwa mifumo ya mifereji ya maji iliyoziba.
Hali mbaya ya mitaa mingi kwa mfano, inatokana na ujenzi wa mifumo ya mifereji ya maji wazi. Mifereji ya maji inakusudiwa kusaidia kuzuia mafuriko, hata hivyo, inapoachwa wazi, taka ngumu zinaweza kujikusanya ndani yake na kusababisha kuziba na kisha kuleta mafuriko ambayo nayo huharibu barabara.
Kiwango cha uchakavu wa barabara huongezeka kutokana na ongezeko la unyevu wa punjepunje na inaonekana wazi kwamba mifereji ya maji iliyo wazi hutumia udongo, ikimaanisha kwamba hakuna lami au njia za watembea kwa miguu, na hivyo mara nyingi punje hizo hukimbilia barabarani na kuwa katika hatari ya kukanyagwa na waendesha magari. Hivyo ni muhimu kuchukua tahadhari kuokoa maisha na mabilioni ya shilingi yanayotumika kutokana na magonjwa na uharibifu unaosababishwa na mifereji ya maji wazi.
Kubuni na kutengeneza mifumo ya mifereji ya maji kunahitaji ushauri wa kitaalamu kutoka kwa wahandisi ili kuhakikisha kuwa maji yanatiririka kwa ufanisi na kwa usalama na yanaelekezwa kwenye mkondo wa maji au njia ya maji. Mifereji ya maji iliyowekwa na jamii moja haipaswi kuleta matatizo kwa jamii nyingine chini ya katika mkondo mmoja, wala haipaswi kuathiri maeneo muhimu ya kiikolojia.
Masuluhisho ya Weholite Stormwater (attenuation tanks & pipes systems) yanatoa njia mbadala endelevu za kutatua changamoto za mafuriko jijini Dar es Salaam, kulingana na wahandisi wanaotekeleza miradi ya miundombinu ya usimamizi wa maji jijini. Weholite hupatikana katika kipenyo cha kati ya DN/ID 350mm hadi DN/ID 3000mm, ambayo yanayafanya kuwa bora kwa kupitishia maji mengi mbali na maeneo yenye matatizo, na hivyo kuwalinda wakazi dhidi ya kadhia ya mafuriko.
Kampuni ya Megapipes hivi karibuni ilisambaza takribani 300m za DN1800 za mabomba ya Weholite, kwa ajili ya mradi mkubwa wa kukabili mafuriko katika Barabara ya Chato, Dar es Salaam. Mfumo huo ulijumuisha makutano ya barabara kukidhi hitaji maalumu la eneo husika na mashimo kwa ajili ya ukarabati/matengenezo, ambayo hutoa suluhisho la muda mrefu dhidi ya tishio la mafuriko mijini.
Usimamizi wa mifumo ya kudhibiti maji ya mvua kubwa katika jiji kubwa si kazi nyepesi wala si kitu kisichowezekana kabisa unapokuwa na masuluhisho ya Weholite ambayo yanatatua baadhi ya changamoto zetu za uhandisi.
Baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na kuweka miundombinu kwa njia ambayo inahatarisha maisha ya wakazi milioni sita wa jiji la Dar es Salaam. Mabomba ya Weholite ni mepesi zaidi kuliko mifumo ile ya zege ambayo hurahisisha usafirishaji na usimamizi wake kuwa sio tu wa haraka lakini nafuu na salama.
Weholite ndiyo bidhaa inayofaa zaidi kwa mifumo ya mifereji ya maji ya mvua kama ile iliyofungwa katika Barabara ya Chato, kutokana na utengamano wake na uwezo wa kubuniwa kwa urahisi katika mipangilio tofauti, ambayo vinginevyo ingekuwa vigumu sana kujenga kwa kutumia mbinu zilizozoeleka. Hii ni sifa muhimu inayohotajika wakati mfumo unapolazimika kukabiliana na changamoto za maeneo ya mijini yenye watu wengi na wingi wa huduma nyingine ambazo ziko chini ya ardhi.
Faida nyingine ni kwamba Kampuni ya Megapipes iliweza kuunganisha na kufanya majaribio ya sehemu zilizojengwa kwenye kiwanda chao Kigamboni, Dar es Salaam na kupunguza muda wa ufungaji miundombinu kwenye eneo la mradi na kuongeza imani kwa mteja. Kwa kuongezea, taka ngumu zinashughulikiwa kwa usalama kupitia hydraulics bora za mifereji ya maji taka iliyofungwa tofauti na ile iliyo wazi.
Mradi wa Barabara ya Chato unaotekelezwa na TARURA Kinondoni unatarajiwa kuboresha maisha ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam ambao wanakabiliwa na mafuriko kila mara. Hivi sasa, mafuriko yanaathiri moja kwa moja na kwa njia isiyo ya moja kwa moja wakazi wawili kati ya watano wa jiji hilo au karibu watu milioni mbili kwa viwango tofauti.
Suluhisho hili jipya na bunifu linaleta thamani kubwa kwa wakazi wa Dar es Salaam, kwa kuwa ni teknolojia iliyotengenezwa nchini na kuthibitishwa, ambayo imekuwa ikitumika duniani kote kuanzia Afrika Kusini, Ulaya na Amerika Kaskazini.
Mustakabali wa usimamizi wa maji
Mabomba na mifumo ya Weholite HDPE inaweza kubuniwa kukidhi ya mtu mmoja mmoja au taasisi katika mazingira yaliyojengwa, au vivyo hivyo kutumika kwenye ujenzi wa haraka wa miundombinu ya usafiri kwenye barabara kuu, barabara za mijini au mazingira ya vijijini; hivyo, kuwaondolea wahandisi changamoto iliyopo ya uwekaji miundombinu nchini.
Kadhia zinazoletwa katika maisha ni mojawapo ya sababu kuu ambazo jamii mara nyingi hupinga utekelezwaji wa miradi mipya, jambo ambalo halipatikani unapotumia bidhaa za Weholite. Yote inamaanisha kwamba teknolojia hii inapaswa kutumiwa kwa uwezo wake wa kufunga miundombinu hii mpya kwa njia ya haraka na ya ufanisi.