Gabon: Kuelekea uchaguzi wa rais bila mshangao?

Wapiga kura wa Gabon wanaitwa kupiga kura Jumamosi, Aprili 12, kwa uchaguzi wa urais ambao unaashiria mwanzo wa kuondoka kipindi cha mpito kilichoanzishwa na mapinduzi ya Agosti 30, 2023. Uchaguzi huo utakuwa na umuhimu wa kihistoria, kwani kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1967, hakuna kadi ya kura itakayo kuwa na jina la “Bongo.” 

Imechapishwa:

Dakika 3

Matangazo ya kibiashara

Kutoka kwa mwandishi wetu maalum huko Libreville,

Wagombea wanane wanachuana katika kinyang’anyiro hicho akiwemo mkuu wa kipindi cha mpito Brice Clotaire Oligui Nguema ambaye amepigiwa upatu na takriban vikosi vyote vya kisiasa na mashirika ya kiraia.

Mbele ya duka la bidhaa karibu na hospitali ya chuo kikuu, marafiki watatu wanakunywa juisi chini ya mwavuli. Marafiki ho hawafichi ukweli kwamba wanathamini utulivu ambao hajapatikani sana wakati wa kipindi cha uchaguzi waliomo kwa sasa.”Tuko hapa, tulivu, hanasikia kwa mbali kuhusu uchaguzi. Hakuna uharibifu, tunakula, tunakunywa, tunalala, ni vizuri sana,” anatabasamu Annie. “Tunasikia maelewano ya watu wa Gabon kwa sasa,” anasema Syntiche, ambaye anasema ana “matumaini makubwa ya amani,” kama Murielle, ” ambaye anasema ana furaha sana “kuepuka kujirudia” kwa migogoro.

Mwaka 2009, 2016 na tena 2023, Gabon iliishi kwa hali ya mikutano, huku upande mmoja PDG (Gabon Democratic Party), chama cha zamani kilichokuwa madarakani kikihangaika kutaka kumbakiza madarakani Ali Bongo kwa kila njia, baada ya babake Omar Bongo kutawala nchi hiyo kwa miaka mingi; na kwa upande mwingine, uhamasishaji wa upinzani kuangusha utawala wa familia ya Bongo, mara nyingi ukishirikiana na waasi. Mwaka huu, hakuna lolote kati ya hayo lililotokea, kwani mlipuko wa kisiasa ulikuwa tayari umetokea mnamo Agosti 30, 2023, wakati jeshi lilipofuta uchaguzi ambao ofisi ya rais wakati huo ilikosa  njia ya kuupindua.

Miezi ishirini baadaye, ni sura ya kiongozi wa wafuasi – wanatumia neno “wakombozi” – ambalo linachukua nafasi ya umma: mabango, kwenye vio vya mabasi, Brice Clotaire Oligui Nguema yuko kila mahali, na kampeni yake ya “C’BON”, ambayo inacheza kwenye herufi zake za kwanza. 

Kampeni ya upendeleo na karibu kuungwa mkono kwa kauli moja kutoka kwa wadau wa kisiasa

Kinachoonekana, kampeni hii ina mwonekano wa kura ya maoni, huku mkuu wa mpito akiwa na rasilimali ambazo ni nje ya uwiano wote wa wapinzani wake. Walakini, wakaazi wengi wa Libreville hawaonekani kuwa na wasiwasi juu yake.

“Wagombea wengine saba hawana wanafanya mikutano na wanategemea mitandao ya kijamii,” anasema wakili Augustin Emane, ambaye. Kwake hakuna kuficha ukweli: “Tuko kwenye kampeni ya kutaka kura za maoni, swali ni je, waliomwangusha Ali Bongo wana haki ya kuendelea. Ni vigumu kupendekeza jambo lingine na kumhoji mtu aliyefanya kitendo hiki ambacho watu wachache walimfikiria na ambacho kilishangiliwa sana. Ikumbukwe kwamba wengi walisema wangempigia kura mbwa kama angemkabili Ali Bongo.”

Kwa kampeni hii, Brice Clotaire Oligui Nguema anafurahia kuungwa mkono na takriban vikosi vyote vya kisiasa, iwe vinatoka katika mfumo wa zamani wa PDG, upinzani wa zamani ambao ulishiriki katika kipindi cha mpito, kama vile viongozi wakuu Alexandre Barro Chambrier au Paulette Missambo, au sauti zilizokuwa zikikosoa sana mashirika ya kiraia kama vile mtetezi wa mazingira Marc Ona Essangui au wakili Kevin N Azisgou.

Kwa hivyo Gabon inamezwa na “C’BON”, na hii sio hatari kwa nchi? “Kampeni iko wazi na inaendelea vizuri, kila mtu anatumia mkakati wake,” amesema Waziri wa Mawasiliano Laurence Ndong. “Mgombea Oligui Nguema ana kauli moja. Watu wanamwona kama mfadhili baada ya wafuasi wa mfumo wa zamani. Lakini pia ana rekodi ambayo inaonyesha taswira ya nchi.” “Watu wa Gabon wametulizwa na ukweli,” anahakikisha mmoja wa wasemaji ishirini na saba wa mgombea huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *