
Rais wa zamani wa Kongo Joseph Kaila Kaange ambaye anaishi rasmi nchini Afrika Kusini tangu mwaka jana, amevunja ukimya na kutangaza kurejea DRC siku ya Jumanne, Aprili 8. Katika taarifa yake iliyoandikwa, amesema anataka kurejea nchini kupitia mashariki, lakini bila kutaja tarehe au eneo kamili. Joseph Kabila anaweza kutegemea watu gani kutekeleza mpango huu? RFI inachambua.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Kwa mujibu wa taarifa zilizokusanywa na RFI, Rais wa zamani wa Kongo Joseph Kabila, ambaye alitangaza kurejea nchini DRC siku ya Jumanne, Aprili 8, amekuwa akipokea wageni wengi mjini Harare, Zimbabwe, ambako amekuwa akiishi tangu mwaka uliopita. Miongoni mwa wageni wake kuna watu wengi kutoka DRC: washiriki wa zamani kwa sehemu kubwa, lakini pia waaminifu wa muda mrefu, bila kutaja watu wengine wengi mashuhurii.
Miongoni mwa wageni hao, jina moja limekuwa likitajwa mara kadhaa : lile laJohn Numbi. Mkuu wa zamani wa polisi ya taifa ambaye baadaye alikuja kuwa Inspekta Jenerali wa FARDC, ambaye anasakwa na mahakama ya kijeshi ya Kongo, haswa kuhusiana na mauaji ya Floribert Chebeya na Fidèle Bazana, ambayo yalimsababisha pia kutafuta hifadhi nchini Zimbabwe. Licha ya kuwa chini ya ombi la kurejeshwa kutoka Kinshasa tangu mwaka 2022, hii haikuzuia kuzungumziwa mwishoni mwa mwaka 2023 kwa kumtishia Rais Félix Tshisekedi hadharani kwenye video kwenye mitandao ya kijamii.
Bado katika upande wa Kongo, vyanzo vilivyowasiliana na RFI vinadai kuwa Joseph Kabila pia anawasiliana na wapinzani waliokimbilia hivi karibuni huko Ulaya – haswa Ubelgiji – na anahesabu miongoni mwa wafuasi wake viongozi kadhaa wa mashirika ya kijamii kutoka mkoa wa Kivu Kaskazini, ambao baadhi yao wanasemekana kuwa na uhusiano na makundi yenye silaha.
“Hakuna uadui” kati ya Joseph Kabila na Paul Kagame
Licha ya mvutano na Rwanda ambao ulisababisha kuanguka kwa utawala wake, Joseph Kabila pia ana mawasiliano na Kigali, ambapo ametuma wajumbe mara kadhaa katika miezi ya hivi karibuni. Kuhusu uhusiano wake na Rais wa Rwanda Paul Kagame, mmoja wa washirika wake wa karibu anabaini kwamba kwa kiasi kikubwa uhusiano wao uko vizuri: “Hakuna uadui” kati yao, anabainisha.
Linasalia suala la Corneille Nangaa: Joseph Kabila ana uhusiano gani na mwenyekiti wa zamani wa CENI ambaye amekuwa mratibu wa AFC/M23, inayopambana na jeshi la Kongo mashariki mwa DRC? Kulingana na mjumbe wa wasaidizi wake, watu hao wawili wanazungumza, lakini hakusema mengi zaidi …
Ikiwa uhusiano kati ya AFC/M23 na Joseph Kabila utathibitishwa, hii itahatarisha utawala wa Félix Tshisekedi, amesema Bob Kabamba, daktari katika masuala ya siasa, mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Liège (Ubelgiji).