
BAO la dakika ya 79 lililofungwa na kiungo Sihle Nduli limetosha kuitupa nje Zamalek ya Misri kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, lakini likiivusha Stellenbosch ikiwafuata Simba.
Ushindi huo wa ugenini wa Stellenbosch unaifanya timu hiyo kukutana na Simba, ikiwazuia wekundu hao kurudi Misri huku ikimrudisha kocha Fadlu Davids kukutana na Wasauzi wenzake.
Simba mapema imepata tiketi ya kufuzu nusu Fainali ya mashindano hayo baada ya kuiondoa Al Masry ya Misri kwa matuta 4-1 baada ya timu hizo kumaliza mchezo kwa u