
Chama kikuu cha upinzani nchini Sudan Kusini kinachoongozwa na makamu wa kwanza wa rais Riek Machar aliyeko kizuizini nyumbani kwake, kimeripotiwa kugawanyika baada ya baadhi ya wanachama kutangaza kumuondoa kama mwenyekiti wa chama.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Mwezi uliopita Machar, aliwekwa kizuizini nyumbani kwake na wanajeshi watiifu wa rais Salva Kiir baada ya mapigano yaliyohusisha wapiganaji vijana wenye uhusiano na kiongozi huyo maarufu kama “white army”.
Na katika hatua inayotazamiwa kuzidisha hali ya taharuki, hapo jana chama chake kilisema kinamteua Stephen Par Kuol kuwa kaimu mwenyekiti wa SPLM –IO kwa muda wakati Machar akiwa bado kizuizini, Kuol akisisitiza kuwa haya si mapinduzi ila ni njia ya kutatua mzozo wa uongozi uliokuwa umesababishwa na kukamatwa kwa Machar.
Hata hivyo Saa chache baadaye upande wa vikosi vya SPLA-IO umesisitiza kuwa bado wataendelea kupkea amri toka kwa Machar peke yake, huku msemaji wa SPLA-IO, Peter Thok Chuol,akisema kuwa naibu wa Machar Nathaniel Oyet Pierino, ataongoza chama hicho kwa muda.
Jumatatu ya wiki hii SPLM-IO ilikuwa imetangaza kusitisha kwa muda uanachama wa Kuol ikimtuhumu kwa kuleta mfarakano na kuwa kibaraka wa Rais Kiir.