Mazungumzo kati ya waasi wa M23 na serikali ya DRC yameahirishwa

Mazungumzo ya amani kati ya serikali ya DRC na waasi wa M23 wanaosaidiwa na Rwanda yaliyokuwa yaanze hapo jana mjini Doha, Qatar, yameahirishwa kwa muda bila hata hivyo ya kutangazwa kwa tarehe nyingine, vyanzo kutoka pande hizo mbili vimethibitisha.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

M23 na serikali ya Kinshasa zilikuwa zimepangiwa kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja na ya kwanza tangu kundi hilo kuchukua udhibiti wa miji mikubwa miwili mashariki ya Congo ya Goma na Bukavu.

Licha ya kwamba haikuwa wazi ni kwa nini mazungumzo hayo yamehairishwa, vyanzo kutoka pande zote vinasema hadi kufikia Jumatatu ya wiki hii, havikuwa vimepokea mwaliko rasmi.

Maelfu ya raia wa mashariki ya DRC wameripotiwa kupoteza makazi yao katika kipindi cha mzozo mpya wa hivi karibuni
Maelfu ya raia wa mashariki ya DRC wameripotiwa kupoteza makazi yao katika kipindi cha mzozo mpya wa hivi karibuni REUTERS – ARLETTE BASHIZI

Aidha vyanzo vilivyokaribu na mchakato wa mazungumzo hayo, mwishoni mwa juma lililopita, vilithibitisha wawakilishi wa pande hizo mbili walikutana juma moja nyuma kwa siri, bila kusema walijadiliana kipi hasa.

Maelfu ya watu wameripotiwa kufariki katika machafuko ya hivi punde mashariki ya DRC wakati mamia ya wengine wakiwa wamepoteza makazi yao.

Wachambuzi wa masuala ya kiusalama wamekuwa wakionya kwamba huenda mzozo huo ukasambaa na kuwa wa kikanda ukihusisha mataifa jirani kama vile Burundi na Uganda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *