
Mashambulio ya jeshi la Israeli, yamewauwa Wapalestina, karibu 30 na kuwajeruhi wengine 60 katika wilaya ya Shejaia, Kaskazini mwa ukanda wa Gaza.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Matangazo ya kibiashara
Madaktari wasiokuwa na mipaka, wanasema, wanajeshi wa Israeli, walishambulia kituo cha afya, eneo ambalo linatarajiwa kuwa salama na kimbilio kwa wakaazi wa Gaza.
Jeshi la Israeli limethibitisha kutekeleza shambulio hilo, ambalo linasema, lililenga ngome kuu ya wapiganaji wa Hamas, na kusababisha vifo hivyo, wengi wakiwa wanawake na watoto.
Israel ilirejelea mashambulio kwenye ukanda wa Gaza, Machi tarehe 18, na kuvunja mkataba wa miezi miwili, uliokuwa umefikiwa kati ya Israeli na kundi la Hamas.
Wapalestina zaidi ya Elfu moja na mia nne, wameuawa tangu kuanza tena kwa mashambulio hayo, na kufikisha idadi ya vifo zaidi ya Elfu 50 tangu kuanza kwa vita hivyo Oktoba mwaka 2023.