RC Chongolo kuondoa changamoto ya foleni ya malori Tunduma

Tunduma. Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo, ameunda kamati maalumu kuchunguza sababu za ucheleweshaji wa malori ya mizigo kuvuka mpaka wa Tunduma, ambapo imebainika baadhi hukaa hadi siku nane yakisubiri vibali vya kuvuka.

Kamati hiyo imeundwa baada ya Chongolo kufanya mazungumzo na wadau wa usafirishaji kwenye kituo cha kutoa huduma kwa pamoja (OSBP) kilichopo mpakani mwa Tunduma, akieleza kuwa ni lazima hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya urasimu na ucheleweshaji unaozikumba shughuli za kuvuka mpaka.

Chongolo ameyasema hayo leo Aprili 9, 2025 huku akiitaka kamati hiyo kutoa mapendekezo ya hatua za haraka leo hii.

Pia, Chongolo ameeleza kuwa, licha ya jitihada za Serikali kutatua changamoto za foleni, changamoto hiyo imeshindikana kupatiwa suluhu ya kudumu.

“Tunataka kujua ni nini kinachosababisha malori kukaa hadi siku nane mpakani. Kila wakati tunapokea changamoto ya foleni katika mpaka wa Tunduma na tunahitaji kubaini chanzo cha tatizo hili,” amesema Chongolo.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo akizungumza wakati wa kikao hicho kuona namna ya kutatua changamoto ya foleni katika Mji wa Tunduma

Pia, amekosoa mawakala wa usafirishaji ambao wamekuwa wakihusishwa na shughuli za kuvusha magari kupelekea upande wa Zambia, wakati kodi za Tanzania tayari zimekusanywa bandarini. Amesema: “Kwa nini mawakala wanahusika kuvusha magari wakati sisi tayari tumekusanya mapato kutoka bandarini? Tunahitaji kujua kwa undani kama nyaraka za magari zilikuwa sawa, na ikiwa kuna ucheleweshaji, ni wapi haswa?”

Chongolo amesema kuwa lengo la kuunda kamati hiyo ni kuongeza ufanisi na kupunguza urasimu katika shughuli za kuvuka mpaka kwa malori ya mizigo, ili kurahisisha na kuharakisha mchakato wa kuvuka.

Mwenyekiti wa Chama cha Madereva wa Masafa Marefu Tanzania, Hassani Debe, ameeleza kuwa wamefanya vikao vingi vya kujadili changamoto ya foleni, lakini matokeo yake hayakuwa na mafanikio ya kudumu.

“Tunatoka Dar es Salaam na nyaraka kamili, lakini tunapofika mpakani, badala ya kutoa nyaraka kwa TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania), tunawapa mawakala, ambao hutoa nyaraka hizo kwa upande wa Zambia. Hii inachangia kuongezeka kwa foleni,” amesema Debe.

Debe ameongeza kuwa foleni katika mpaka wa Tunduma ni ya kutengeneza.

Amesema, “Foleni hii inaisha mara tu wanapojua watu wamekuja. Tunajiuliza, kama sio ya kutengeneza, kwa nini foleni inaisha tukiondoka na kisha kurudi tena? Hii inahitaji uchunguzi wa kina.”

Ramadhani Selemani, mfanyakazi wa Chama cha Madereva Tanzania, ameeleza kwamba moja ya sababu kubwa ya foleni ni milolongo ya nyaraka kupitia mawakala.

Amehoji, “Mawakala hawa wanapaswa kutueleza ni kwa nini wanahusika na shughuli ambazo zinachangia ucheleweshaji wa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *