Penalti ya Pamba Jiji yamshangaza Minziro

KITENDO cha Pamba Jiji kupewa mkwaju wa penalti dakika ya 90+7 kisha kukosa ilipotoka sare ya 1-1 na Fountain Gate, kimemshangaza zaidi kocha wa timu hiyo, Fredy Felix ‘Minziro’.

Penalti hiyo ilipatikana baada ya beki wa Fountain Gate kumgonga mguuni James Mwashinga katika harakati za kuokoa juzi, mpigaji Mathew Tegis akagongesha mwamba wa juu na kurudi uwanjani kabla ya kufanya shambulizi lingine lililotoka nje na mchezo kumalizika.

Minziro alishangazwa na namna wachezaji wake walivyoonyesha kukataa kupiga mkwaju huo kabla ya Tegis kuchukua jukumu hilo kama alivyofanya dakika ya 22 alipofunga bao la kwanza kwa penalti, lakini ile ya pili bahati haikuwa kwake, akakosa.

‘Vijana wangu kujiamini kumepungua sababu tayari Tegis alishakataa kupiga penalti.. sasa yeyote angeenda kuchukua mpira akapiga.

“Ni kweli tulimuandaa Tegis na penalti ya kwanza alifunga, hii ya pili akakosa kujiamini na bahati mbaya wote wameiogopa kuipiga. Pengine yeyote angepiga vizuri.

“Wapo wapigaji wengi tu kama Mwashinga (James) lakini sijajua kwa nini wameogopa kupiga penalti. Tulishatangaza kwamba mpigaji atakuwa Tegis alipofunga ya kwanza tulitegemea ya pili pia ajiami

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *