Tadesse Werede ndiye kiongozi wa mpito katika jimbo la Tigray Ethiopia

Serikali ya Ethiopia, imemteua Tadesse Werede, kuwa kiongozi mpya wa mpito katka jimbo la Kaskakzini la Tigray, kufuatia mivutano ya uongozi kati ya makundi mawili, yanayotishia kuvunjika kwa mkataba wa amani wa mwaka 2022.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya kushuhudiwa kwa mivutano kati ya aliyekuwa kiongozi wa jimbo hilo Getachew Reda, na kiongozi wa kikosi cha Tigray People’s Liberation Front (TPLF) Debretsion Gebremichael.

Katika harakati za kujaribu kutuliza na kuepuka mgawanyiko zaidi, Waziri Mkuu Abiy Ahmed, ameteua Werede, ambaye alikuwa naibu wake Reda, kushika nafasi hiyo.

Kiongozi huyo mpya amehidi kuongoza kwa weledi na kuhakikisha kuwa watu wanaomiliki wanazirejesha, kurejesha watu waliokimbia makaazi yao kwa sababu ya vita na kuandaa jimbo la Tigray kushiriki kwenye uchaguzi.

Waziri Mkuu Abiy, kupitua ukurasa wake wa kijamii wa X, ameandika kuwa, mabadiliko ya madaraka yamefanyika kwa amani na kiongozi huyo mpya ana ufahamu mkubwa wa changamoto zinazowakabili wakaazi wa Tigray.

Wachambuzi wa masuala ya Ethiopia, wamekuwa wakisema kiongozi wa zamani Getachew, alikuwa anapoteza maeneo mbalimbali katika jimbo hilo, baada ya kundi lenye silaha linaloongozwa na Debretsion kudhibiti mji wa Adigrat na hivyo kulikuwa na umuhimu mkubwa wa mabadiliko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *