SPLA-IO yapuuza agizo la kutobeba silaha kwenye maeneo ya umma Sudan Kusini

Kikosi cha SPLA-IO chake Makamu wa kwanza wa rais wa Sudan Kusini Riek Machar aliyekamatwa  na kuzuiwa nyumbani kwake mwishoni mwa mwezi uliopita, kinawataka wapiganaji wake kupuuza agizo la jeshi la taifa kuwataka wasibebe wala kutembea na silaha katika maeneo ya umma.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Wito huu unakuja  baada ya jeshi kutoa agizo hilo na kuwataka wapiganaji hao wa Machar, kurejea katika maeneo yao ya kazi, ikiwemo kwenye kambi za  jeshi.

Hata hivyo, watu wa karibu wa Machar, wamevitaka vikosi hivyo, kuendelea kujihami na kuwa makini wakati wote, katika maeneo yake yote wanayodhibti.

Kukamatwa kwa Machar ambaye rais Salva Kiir amemtuhumu kwa kuwaunga mkono waasi wa White Army, walioshambulia kambi ya jeshi katika jimbo la Upper Nile, kunatishia kurejesha nchi hiyo kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Inahofiwa kwamba huenda kukawa na mpasuko kwenye serikali kati ya upande wa rais Salva Kiir na ule wa Riek Machar.
Inahofiwa kwamba huenda kukawa na mpasuko kwenye serikali kati ya upande wa rais Salva Kiir na ule wa Riek Machar. © Ben Curtis / AP

Mbali na Machar, washirika wake wengine zaidi ya 20 wakiwemo wanasiasa na wanajeshi wamekamtwa.

Wajumbe kutoka Umoja wa Afrika waliozuru Juba wiki iliyopita, wamependekeza kuachiwa huru kwa Machar na washirika wake na suluhu ya mzozo huo kupatikana kwa njia ya mazungumzo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *