
China imeapa kupambana mpaka mwisho, kufutia tisho la rais wa Marekani Donald Trump kusema kuwa, anaweza kuongeza kiwango cha utozwaji wa kodi wa bidhaa zake kutoka asilimia 34 ya sasa hadi asilimia hamsini.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
China ni mshirika mkubwa kibiashara wa Marekani na imelaani kauli hiyo ya Trump, iliyosema ni vitisho, kuelekea utekelewaji wa hatua ya kiongozi huyo wa Marekani wiki iliyopita, kutangaza kuwa bidhaa zote kutoka China zinazoingia katika nchi hiyo, zitatozwa ushuru wa asilimia 30 kuanzia Jumatano saa sita usiku.
Wizara ya biashara ya China nayo imesema, itatoza bidhaa kutoka Marekani asilimia 34 ya ushuru kama njia ya kulipiza kisasi, kauli ambayo imeonekana kumkera Trump ambaye ametishia nyongoza zaidi ya ushuru kwa Beijing.
Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya, amezungumza na Waziri Mkuu wa China Li Qiang na kuonya dhidi ya kuendeleza mzozo wa kibiashara hasa kati ya Marekani na China.
Trump pia ametangaza nyongeza ya ushuru kwa bidhaa kutoka nchi za Ulaya, ambazo sasa zitatozwa asilimia 20 zitakapoingia Marekani.
Ushuru wa asilimia 10 kwa bidhaa kutoka mataifa mengine ya dunia, ulianza kutozwa Jumamosi iliyopita, hatua ambayo imetikisa bishara kwenye masoko ya fedha katika mataifa mbalimbali duniani.