Masika yasimamisha ligi ya kikapu Arusha

MVUA za masika zinazoendelea kunyesha mjini Arusha zimeathiri kuanza kwa mashindano ya Ligi ya Kikapu mkoani humo msimu ujao.

Awali, Chama Mpira wa Kikapu Mkoa Arusha (ARBA) kilipanga kukutana na viongozi wa klabu shiriki ili kukubaliana tarehe ya kuanza mashindano hayo baada ya kushindwa kuanza kutokana na mvua zinazonyesha.

Jackob Gibons, mwenyekiti wa ARBA ameliambia Mwanaspoti kwamba, uongozi wa ARBA ulipanga kukutana na viongozi wa klabu, lakini hadi sasa wameshindwa kutokana na mvua zinazonyesha, kwani hata wakikutana mashindano hayataanza hivi karibuni.

“Kipindi hiki cha masika imekuwa ni ngumu kukutana na viongozi wa klabu kupanga tarehe ya kuanza kwa Ligi. Tunasubiri masika ikimalizika tutafanya kikao na viongozi wa klabu kabla ya kupanga tarehe ya kuanza kwa ligi tutapitia kanuni, ” alisema Gibson.

Mwenyekiti huyo alisema ugumu wa kuanza kwa ligi unatokana na viwanja vinavyotarajiwa kutumikia ambavyo vimeathiriwa na mvua hizo na pia ni vya wazi. Kwa wanaume bingwa mtetezi wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Arusha ni Pamoja na kwa wanawake ni Arusha Queens.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *