
China imeliapa Jumanne kupambana na ushuru wa forodha wa Marekani “hadi mwisho” licha ya tishio la Donald Trump la kutozwa ushuru mpya, huku mataifa hayo mawili yenye uchumi mkubwa duniani yakisema kuwa yamejiandaa ka kuongezeka kwa mgogoro licha ya kudorora kwa soko la fedha.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Utawala wa Marekani umehakikisha kuwa bado uko wazi kwa mazungumzo.
Hatari za kuongezeka kwa vita vya kibiashara vya pande zote zinaendelea, huku Donald Trump akiikosoa Beijing kwa “kutozingatia (…) onyo (…) la kutolipiza kisasi.”
Ametishia kutoza ushuru mpya wa hadi 50% kwa bidhaa za China mapema Jumatano ikiwa Beijing itaendelea katika jaribio lake la kutoza ushuru mpya wa 34% kwa bidhaa za Marekani.
“China haitakubali kamwe hii,” msemaji wa Wizara ya Biashara amesema. “Ikiwa Marekani itasisitiza juu ya hili, China itapambana nayo hadi mwisho,” ameongeza, akisisitiza, hata hivyo, kwamba angelipendelea “mazungumzo” na Marekani.
Tangu arudi White House mnamo mwrzi wa Januari, Donald Trump tayari ameweka ushuru mpya wa 20% kwa bidhaa za China. Unatarajiwa kuongezeka hadi 54% kutoka Aprili 9, na +34% iliyotangazwa wiki iliyopita.
Iwapo atatekeleza tishio lake la hivi punde, itaongeza malipo hayo hadi asilimia 104, na hivyo inatosha kuongeza maradufu bei ya bidhaa za China zinazoingia Marekani.
Kiongozi wa Hong Kong John Lee ametaja ushuru huo kama “kutowajibika.”
– Mfumuko wa bei zaidi, ukuaji mdogo –
Katika muda wa hivi karibuni, China inataka kutuliza dhoruba ya kifedha iliyosababishwa na hatua hizi na benki yake kuu imeahidi kuunga mkono hazina kuu ya serikali ya China, Central Huijin Investment, ili kuleta utulivu wa masoko.
Soko la hisa la Hong Kong liliongezeka kwa karibu 2% mwanzoni siku ya Jumanne, siku moja baada ya kuanguka vibaya zaidi tangu msukosuko wa kifedha wa mwaka 1997 (-13%), wakati soko la hisa la Shanghai lilipanda kidogo.