
Baada ya zaidi ya miezi minane ya mgogoro ambao haujawahi kushuhudiwa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Noël Barrot ameweza kukutana Jumapili, Aprili 6, mjini Algiers na mwenzake wa Algeria, Ahmed Attaf, na Rais wa Algeria Abdelmajid Tebboune.
Imechapishwa:
Dakika 3
Matangazo ya kibiashara
Mwishoni mwa “majadiliano haya ya kina, ya wazi na yenye kujenga” ambayo yalichukua saa kadhaa, waziri alitangaza “kuhuisha tena taratibu zote za ushirikiano” kati ya Ufaransa na Algeria, katika njanja za usalama, uhamiaji, haki na mahusiano ya kiuchumi.
Siku ya Jumapili hii, Aprili 6, mjini Algiers kulishuhudiwa ufunguzi wa awamu mpya katika uhusiano kati ya Ufaransa na Algeria. Wakati wa mazungumzo yake ya zaidi ya saa mbili na nusu na rais wa Algeria, Jean-Noël Barrot ameweza “kueleza kanuni” ambazo tayari zimetajwa na Marais Emmanuel Macron na Abdelmajid Tebboune wakati wa mazungumzo yao ya simu. Jean-Noël Barrot amezungumza kwa ufupi alipokuwa akiondoka kwenye Ikulu ya El Mouradia.
“Nilitaka kuheshimu mwaliko huu haraka iwezekanavyo, chini ya wiki moja baada ya mazungumzo ya simu kati ya Marais Macron na Tebboune na taarifa yao ya pamoja. “Tumepitia kipindi cha mvutano usio na kifani katika miezi ya hivi karibuni ambao haujali maslahi ya Waalgeria au Wafaransa,” Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa ametangaza.
Hakika tuna tofauti, lakini uhusiano unaotuunganisha lazima utuongoze kuanza tena mazungumzo na kuanzisha tena ushirikiano.
“Hakika tuna tofauti, hatuwezi kuzipuuza, lakini uhusiano wa kibinadamu, kihistoria na kiutamaduni unaotuunganisha lazima utuongoze kuanza tena mazungumzo na kuanzisha tena ushirikiano. Uhusiano wetu wa kitaasisi lazima uwe sawa na uhusiano wa kibinadamu kati ya nchi zetu mbili. Nilikuja Algiers kutoa ujumbe wa Rais wa Jamhuri. “Ufaransa inataka kufungua ukurasa kuhusu mivutano iliyopo na kujenga upya ushirikiano wa amani na usawa na Algeria,” ameongeza.
Mikutano ijayo ya nchi mbili
“Tumeweka wazi juu ya meza masuala yote ambayo yametuhusu katika miezi ya hivi karibuni. “Tumeamua kufanya hivi kwa umakini, kwa busara na kwa ufanisi, kwa kufufua upya mifumo yote ya ushirikiano katika sekta zote leo,” ametangaza Jean-Noël Barrot.
Msururu wa mikutano baina ya nchi hizo mbili katika ngazi zote utafanyika katika wiki zijazo kati ya wawakilishi wa Ufaransa na wa Algeria kwa kurasimisha kuanzishwa tena kwa kazi hii.
Mkutano wa maafisa wa juu zaidi wa usalama wa nchi zetu mbili sasa umepangwa na, vivyo hivyo, tutakuwa na mazungumzo ya kimkakati juu ya Sahel,” ameongeza Jean-Noël Barrot, wakati katika nyanja ya kiuchumi, mkuu wa Medef atampokea mwenzake wa Algeria mnamo Mei 9, mzozo wa miezi michache iliyopita ukiwa umepunguza kasi ya biashara kati ya Ufaransa na Algeria.
“Nilipata fursa ya kukumbusha matatizo ambayo yametokea katika miezi ya hivi karibuni kuhusu maendeleo ya biashara yetu maalum katika sekta ya kilimo cha chakula, magari na usafiri wa baharini. Rais Tebboune amenihakikishia nia yake ya kuwapa msukumo mpya,” pia ameonyesha Jean-Noël Barrot, ambaye pia ameelezea mpango wake kwa ajili ya kuanza tena kwa ushirikiano katika masuala ya uhamiaji. “Rais Tebboune ameonyesha kwamba alikuwa akiunga mkono mkutano ujao kati ya mabalozi wa Algeria nchini Ufaransa na wakuu,” ameeleza kabla ya kuendelea: “Tulikubaliana kufanyia kazi yaliyomo katika makubaliano ambayo yanasimamia uhusiano wetu juu ya uhamiaji na kubaini maboresho muhimu ili kuifanya iwe na ufanisi zaidi.”
Hatimaye, majadiliano pia yataanza tena kuhusu suala la kumbukumbu, mkuu wa diplomasia ya Ufaransa amesema, akiongeza kuwa mwanahistoria Benjamin Stora amealikwa Algiers kuendelea na kazi yake ya kurejesha mali ya kihistoria. Jean-Noël Barrot amehitimisha hotuba yake kwa neno kwa mwandishi wa Ufaransa mwenye asili ya Algeria Boualem Sansal, akitoa wito kwa mara nyingine “ishara ya ubinadamu kutokana na umri wake na hali yake ya afya.”