
ACHANA na msimamo ulivyo wa Ligi ya Wanawake, JKT Queens ikiwa kileleni na pointi 38, timu hiyo inaongoza kwa kutoa vichapo kama ilivyo kauli mbiu yao ‘Kichapo cha Kizalendo’.
Msimu huu imetoa vipigo vitanpo hadi sasa sawa na ilivyotoa msimu uliopita wote na tayari imefunga mabao 56 ikiwa timu pekee iliyofunga mabao kuanzia 50 kwenye mechi 14, huku Simba ikiweka kambani 46 tofauti ya mabao 10.
Msimu huu timu hiyo ikiwa kwenye mbio za ubingwa imezifunga baadhi ya timu mabao kuanzia mabao matano na kuendelea kama ilivyokuwa msimu wa kwanza ulipochukua ubingwa.
12-0 Mlandizi Queens Februari 04
5-0 Mashujaa Queens Machi 19
5-0 Ceasiaa Queens Machi 23
7-0 Mlandizi Queens
6-0 Ceasiaa Queens
Hii sio mara ya kwanza kwa timu hiyo kutoa vichapo hivyo, kwani ishafanya hivyo msimu uliopita ilipomaliza ligi ikifunga mabao 54 na kuruhusu saba.
Kiufupi msimu huu zikiwa zimesalia mechi nne, tayari timu hiyo imevunja rekodi ya msimu uliopita na safu ya ushambuliaji msimu huu inaonekana kuwa bora zaidi ikifunga mabao hayo huku ikisubiriwa kama itatoa kichapo kingine kikubwa na kuipita rekodi ya msimu uliopita.
Msimu 2017/18, ndiyo mwaka ambao JKT ilinyakua ubingwa wa WPL kwa mara ya kwanza ilipotoa vipigo vya mabao matano au zaidi kwa baadhi ya timu ikiwamo Simba Queens.
Novemba 26, 2017
JKT Queens 9-0 Mlandizi Queens
Asha Mwalala (manne)
Fatuma Mustafa (mawili)
Stumai Abdallah
Donisia Minja
Anna Katunzi
Novemba 29, 2017
JKT Queens 9-0 Fair Play
Hat-trick kila mmoja
Asha Mwalala
Stumai Abdallah
Fatuma Mustafa
Desemba 3, 2017
JKT Queens 5-0 Evergreen Queens
Donisia Minja
Asha Mwalala (mawili)
Fatuma Mustafa
Stumai Abdallah
Desemba 6, 2017
JKT Queens 5-1 Mburahati Queens
Fatuma Mustafa (mawili)
Stumai Abdallah (hat-trick)
Desemba 9, 2017
JKT Queens 5-2 Simba Queens
Asha Mwalala (mawili)
Stumai Abdallah
Fatuma Mustafa
Fatuma Mwisendi