
KMC imeondoka na pointi tatu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons ikiitandika mabao 3-2 kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar.
Mchezo huo uliopigwa saa 10:15 jioni ya leo, ilishuhudiwa mshambuliaji wa KMC, Shaban Idd Chilunda akifunga mabao mawili dakika 42 kwa penati na dakika ya 67. Lingine lilifungwa na Ibrahim Ahmed dakika 55.
Katika harakati za kupambana isipokee kichapo hicho, Haruna Chanongo aliifungia Tanzania Prisons mabao mawili dakika ya 64 na 84 ambayo hayakutosha kuwapa hata pointi moja.
Kabla ya mchezo huo, KMC ilikuwa nafasi ya 11, sasa imepanda hadi ya tisa ikifikisha pointi 27, huku Tanzania Prisons ikisaliwa nafasi ya 15 na pointi 18.
Kwenye mechi 24 ilizocheza Tanzania Prisons, imeshinda nne, sare sita na kupoteza 14, KMC kwenye mechi hizo imeshinda saba, sare sita na kupoteza 11.