
Rais wa Urusi Vladimir Putin siku ya Ijumaa Maachi 28 ametoa wazo la “utawala wa mpito” kwa Ukraine, chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa, ili kuandaa uchaguzi wa rais wa “kidemokrasia” nchini na kisha kujadili makubaliano ya amani na mamlaka mpya.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
“Bila shaka tunaweza kujadiliana na Marekani, hata na nchi za Ulaya, na bila shaka na washirika wetu na marafiki, chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa, uwezekano wa kuanzisha utawala wa mpito nchini Ukraine,” Vladimir Putin ametangaza wakati akizuru Murmansk, kaskazini magharibi mwa nchi.
“Katika muktadha wa shughuli za kulinda amani za Umoja wa Mataifa, tayari tumetumia kile kinachoitwa utawala wa mpito mara kadhaa,” ameongeza kiongozi huyo wa Kremlin, akikumbusha hasa kesi ya Timor Mashariki mwaka 1999. Kauli hiyo imekuja wakati washirika wa Ukraine wa Ulaya walipokutana mjini Paris siku ya Alhamisi kujadili “dhamana” za usalama kwa Kyiv, huku Uingereza na Ufaransa zikiweka mbele mipango ya kutumwa kwa kikosi nchini Ukraine ambayo imekuwa ikikabiliana na mashambulizi ya Urusi tangu zaidi ya miaka mitatu.
Washington, ambayo inataka kupata usitishaji vita nchini Ukraine kwa gharama yoyote, imefanya maelewano ya kuvutia na Moscow, na kuwafanya Ukraine na nchi za Ulaya kuogopa makubaliano yasiyo kuwa na msingi.
Vikosi vya Urusi vina “mpango wa kimkakati” kwenye mstari mzima wa mbele huko Ukraine, kiongozi wa Kremlin pia amebainisha.
“Katika mstari mzima wa mbele, vikosi vyetu vina mpango wa kimkakati (…) “Kuna sababu za kuamini kwamba tutawamaliza,” Putin amesema wakati alipokuwa akizuru Murmansk kaskazini magharibi mwa nchi, akiongeza kuwa “watu wa Ukraine wenyewe wanapaswa kuelewa kinachotokea.”