Mpango wa madini kati ya DRC na Marekani wakosolewa na wanaharakati

Mpango wa serikali ya DRC chini ya rais wa DRC Felix Tshisekedi, kuingia kwenye mkataba na nchi ya Marekani kuhusu madini ya nchi hiyo, umezua upinzani mkali kutoka kwa wanaharakati na wakaazi wa Mashariki mwa nchi hiyo.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya mashirika hayo ya kiraia jijini Goma yamemulaumu Raisi Felix Tshisekedi, kutokushirikisha pande zote za upinzani katika utawala bora nchini DRC.

Lumumba Muisa ni mmoja wa waliotoa malalamiko yao jijini Goma.

‘‘Tunasema kuwa Tshisekedi aondoke madarakani na Marekani na Trump na nchi yake wasikubakili mambo hayo ya madini, kwani sio kwa sababu za kuijenga nchi bali ni kwa ajili ya maslahi binafsi ya Tshisekedi .’’ alisema Lumumba Muisa mmoja wa waliotoa malalamiko yao jijini Goma

Baadhi ya raia wa kawaida wametoa mtazamo wao kuhusiana na suala hili.

‘‘Sisi tunahitaji amani, hatukubali fujo tumechoshwa na maneno tu ambayo hayawezi kuwa suluhisho la kupata amani kwa sababu tangu zamani yalichukuliwa madini lakini hadi sasa tunateswa hatuna amani.’’ Alisema mmoja wa raia wa DRC.

Mchambuzi wa maswala ya usalama Justin Mwanatabu ameitaka Kinshasa kuwa tayari kutilia maanani mahitaji ya mashirika ya kiraia, kama njia ya kuhimarisha usalama DRC.

‘‘Shirika la kiraia lina haki ya kuipaza sauti, kwa sababu walitoa mapendekezo kadhaa kwa serikali ya Kinshasa lakini hakuna yalioyotiliwa maanani.’’ Alisema Mchambuzi wa maswala ya usalama Justin Mwanatabu.

Haya yanajiri wakati huu wakuu kutoka Jumuia ya Afrika mashariki EAC na SADC, wakendeleleza juhudi za kupatikana kwa  amani na usalama mashariki mwa  DRC.

CHUBE NGOROMBI GOMA RFI KISWAHILI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *