Korea Kusini: Mahakama ya Kikatiba yakataa kutimuliwa kwa Waziri Mkuu Han Duck-soo

Mahakama ya Kikatiba ya Korea Kusini siku Jumatatu, Machi 24, imetupilia mbali ombi la kutimuliwa kwa Waziri Mkuu Han Duck-soo, huku kukiwa na mzozo wa kisiasa ambao umetikisa nchi hiyo kwa miezi minne. Kwa hivyo Waziri Mkuu Han Duck-soo anakuwa rais wa mpito tena wakati akisubiri kujua hatima ya Yoon Suk-yeol, ambayeanalengwa na utaratibu huo, shirika la habari la Yonhap limebainisha.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Huu ni ushindi mdogo kwa wafuasi wa Rais Yoon: Waziri Mkuu wake Han Duck-soo anarejea ofisini mara baada ya uamuzi wa Mahakama ya Kikatiba asubuhi ya leo, anaripoti mwandishi wetu wa Seoul, Celio Fioretti. “Kesi za kumuondoa Han zilikataliwa kwa kura ya watano kwa mmoja na majaji wanane wa mahakama,” kulingana na shirika la habari la Yonhap. Bw. Han alisimamishwa kazi na wabunge mwezi Desemba baada ya muda mfupi.

Korea Kusini imetumbukia katika machafuko ya kisiasa tangu mapinduzi ya rais aliyeko madarakani, Yoon Suk-yeol, usiku wa Desemba 3 kuamkia Desemba 4. Mwendesha mashtaka huyo nyota wa zamani alitangaza sheria ya kijeshi kwa mshangao na kupeleka jeshi bungeni katika jaribio la kunyamazisha wabunge. Lakini idadi ya kutosha ya wabunge waliweza kukusanyika ili kuzuia haraka mipango yake kwa kupiga kura kwa kauli moja kurejea kwa utawala wa kiraia. Kwa kulazimishwa na Katiba, Yoon Suk-yeol alilazimika kutii.

Mnamo Desemba 14, wabunge hao walipigia kura hoja ya kwanza ya kumtimua kiongozi huyo ambaye alisimamishwa kazi. Kisha tarehe 27 dhidi ya mbadala wake wa kwanza, Han Duck-soo, akishutumiwa kwa kuzuia kesi dhidi ya rais. Han Duck-soo pia alilengwa na kesi kwa sababu ya kukataa kuteua majaji katika Mahakama ya Kikatiba.

Hadi uamuzi wa Mahakama ya Kikatiba mnamo Jumatatu, Waziri wa Fedha Choi Sang-mok alikuwa akikaimu kama rais wa muda, na kisha kuwateua majaji husika. Majaji hawa wanachukulia hatua ya Han Duck-soo kuwa ukiukaji wa sheria, lakini si nzito vya kutosha kutoa kibali cha kuachishwa kazi.

Uamuzi unakaribia kwa Yoon Suk-yeol

Wakati uamuzi wa mahakama kuhusu Han Duck-soo unawatia nguvu wafuasi wa Rais Yoon, waziri mkuu hakuhusika moja kwa moja katika jaribio la kuweka sheria ya kijeshi na majaji waliamua tu mzozo wa kiutaratibu. Kwa hivyo ni vigumu kusema kama Rais Yoon Suk-yeol pia atapata hukumu nzuri.

Wataalamu wanatabiri hukumu kutoka kwa Mahakama ya Kikatiba katika siku zijazo, lakini tarehe kamili haijatangazwa. Iwapo majaji watatangaza kuachishwa kwake kazi, itabidi uchaguzi mpya wa urais uandaliwe ndani ya siku 60. Vinginevyo, atarejeshwa.

Yoon Suk-yeol pia anakabiliwa na kesi ya jinai sambamba kwa “uasi” kufuatia kuwekewa kwake sheria fupi ya kijeshi. Alikamatwa mapema mwezi Januari na kisha kuwekwa kizuizini, kabla ya kuachiliwa Machi 8 kutokana na makosa ya utaratibu. Nchini Korea Kusini, uasi ni uhalifu unaoadhibiwa kwa kifungo cha maisha au hata hukumu ya kifo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *