
Dar es Salaam. Jeshi la Polisi limetangaza nafasi za ajira kwa vijana wa Kitanzania wenye elimu ya shahada, stashahada, astashahada, kidato cha sita na cha nne wenye sifa mbalimbali.
Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Camilius Wambura, Machi 20, 2025 vijana wanaohitajika wanatakiwa kuwa raia wa Tanzania kwa kuzaliwa, wazazi wawe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa na awe amehitimu kidato cha nne au cha sita kuanzia mwaka 2019 hadi 2024.
Sifa nyingine ni waombaji wa kidato cha nne, cha sita na wenye astashahada awe na umri kuanzia miaka 18 hadi 25, kwa waombaji wa kidato cha nne wawe na ufaulu wa daraja la kwanza mpaka la nne.
Kwa waombaji wenye ufaulu wa daraja la nne wawe na ufaulu wa alama 26 hadi 28, huku waombaji wa kidato cha sita wawe na ufaulu wa daraja la kwanza hadi la tatu. Wahitimu wa shahada na stashahada wawe na umri kuanzia miaka 18 hadi 30, urefu usiopungua futi tano na inchi nane (5’8”) kwa wanaume na futi tano inchi nne (5’4”) kwa wanawake.
Sifa nyingine ni kuwa na kitambulisho cha Taifa au namba ya utambulisho kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), uwezo wa kuongea Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha na afya njema kimwili na kiakili iliyothibitishwa na daktari wa Serikali.
Muombaji anatakiwa kuwa hajaoa, kuolewa au kuwa na mtoto ama watoto, hajawahi kutumia dawa za kulevya za aina yoyote, kuwa tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya taaluma ya Polisi na awe hajaajiriwa au hajawahi kuajiriwa na taasisi nyingine ya Serikali.
Anatakiwa kuwa tayari kufanya kazi za Polisi mahali popote Tanzania, kujigharimia katika hatua zote za usaili endapo ataitwa kwenye usaili, asiwe na alama za kuchorwa mwilini (tattoo) wala kumbukumbu za uhalifu.
Kwa waombaji wenye elimu ya kiwango cha shahada (NTA level 8), stashahada (NTA level 6) na astashahada (NTA Level 5 au NVA Level 3) wanatakiwa kuwa na fani zilizoainishwa kwenye tangazo la nafasi za ajira.
Waombaji wote wanatakiwa waandike barua za maombi wao wenyewe kwa mkono bila kusahau namba za simu na watumie anuani ya Mkuu wa Jeshi la Polisi S.L.P 961 Dodoma. Barua hiyo iambatishwe kwenye maombi ikiwa kwenye mfumo wa ‘pdf’.
Waombaji wote wanatakiwa wafanye maombi kupitia kwenye mfumo wa Ajira wa
Polisi (Tanzania Police Force – Recruitment Portal)
unaopatikana kwenye kiunganishi (link) cha tovuti ya Jeshi la Polisi
(https://ajira.tpf.go.tz).
“Maombi yatakayowasilishwa kwa njia ya posta, barua pepe (email) au kwa mkono hayatapokelewa,” limeeleza tangazo hilo.
Mwisho wa kupokea maombi ni Aprili 4, 2025.
Fani zinazohusika
Fani zinazotakiwa kwa kila ngazi ya elimu kwa upande wa Tanzania Bara kwa wenye shahada ni Anesthesia, Animal science, Anthropology, Architecture, Automobile, Engineering, Biology, Biomedical Engineering, Biotechnology and Laboratory Science, Botany, Civil Engineering, Computer Engineering, Computer Information System, Computer Network and Security Engineering, Computer Science, Cyber Crime and Cyber Security, Cyber Forensic and Cyber Security, Database Administration, Electrical Engineering, Film and Video Production; French, Portuguese, Chinese and Arabic na General Agriculture.
Zingine ni Gynecology, Journalism And Mass Communication, Land Management and Evaluation, Law Enforcement, Marine Engineering, Marine Transportation and Nautical Science, Mechanical Engineering, Medical Doctor, Medical Laboratory, Multimedia Content, Network Engineering, Nursing, Pediatrician, Pharmacy, Physiotherapy, Psychiatric Nurse, Quantity Surveyor, Radiology, Range Management, Real Estate, Records and Archive Management, Shipping and Logistics Management, Sign Language/Special Needs, Software Engineering, Statistics, System Development, Tax Management, Telecommunication and Electronics Engineering, Translation and Interpretation na Veterinary Medicine.
Wenye stashahada fani zinazohusika ni Animal Health and Production, Auto Electrical Engineering, Cartography, Clinical Dentistry, Clinical Medicine, Forensic Science, Graphic Design, Multimedia and Animation, Information and Communication Technology, Masterfisherman, Music, Nursing and Midwifery, Optometrist, Performing and Visual Arts, Radar Operation, Sound Engineering na Wildlife Management.
Kwa wenye astashahada fani husika ni Air Conditioning and Refrigeration, Aluminum and Glass Working, Autobody Repair, Aviation Quality Manager, Aviation Safety Manager, Boat Painting, Boat Skippers for Autobody Engineering, Car Interior Design, Car Paint Technician, Carpentry and Joinery, Clearing and Forwarding, Divinity, Drone Operation, Electrical Installation, Excavator Operation, Film Production, Fitter and Turner, Forensic Science, Hydraulic and Pneumatic Mechanics, Industrial Electrical Engineering, Islamic Knowledge; Judo, Karate, Boxing and Taekwondo, Laboratory Technician, Mandatory Courses, Marine Electrical Engineering na Mason and Brick Laying.
Zingine ni Medical Records, Motor Cycle Mechanics, Motor Rewinding, Motor Vehicle Mechanics, Offset Printing, Paintings and Sign Writing, Performing and Visual Arts, Plumbing and Pipe Fittings, Printing Machine Operation, Radio or Electronics and Communication Technology, Rating Part Engineering, Rating Part Navigation, Scuba Diving, Sewing Machine Maintenance, Tailoring, Truck and Heavy Duty Mechanics, Veterinary Laboratory na Welding and Fabrications.
Fani zinazotakiwa kwa kila ngazi ya elimu Zanzibar kwa upande wa shahada ni Accounting and Finance, Civil Engineering, Computer Science, Electronics and Telecommunication, Geography and Environmental Studies, Insurance and Risk Management, Journalism And Broadcasting, Law/Law Enforcement, Medical Doctor, Medical Laboratory, Multimedia Technology, Nurse, Pharmacy, Procurement and Supply Management, Psychiatrist na Radiology.
Wenye stashahada wanatakiwa kuwa na fani ya Animal Health and Production, Civil Engineering, Clinical Medicine, Computer Science, Counselling and Psychology, Electrical Engineering, Electronics and Telecommunication, Hospitality and Tourism Management, Human Resource Management, Information and Communication Technology, Mechanical Engineering, Medical Laboratory, Nursing and Midwifery, Pharmaceutical Science, Physiotherapy, Record and Archives Management, Science With Education na Sign Language.
Kwa wenye astashahada wanatakiwa kuwa na fani za Carpentry and Joinery, Driving, Electrical Installation, Hotel Management, House Keeping, Mason and Brick Laying, Plumbing and Pipe Fittings na Tailoring.