
Serikali ya Israeli imetangaza leo Ijumaa, Machi 21, kumfukuza kazi Ronen Bar, mkuu wa Shin Bet – idara ya usalama wa ndani ya Israel – ambaye Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu amesema hana imani naye tena.
Imechapishwa:
Dakika 3
Matangazo ya kibiashara
“Serikali imeidhinisha kwa kauli moja pendekezo la Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu la kusitisha mamlaka” ya Ronen Bar, ambaye ataondoka madarakani mrithi wake atakapoteuliwa au hivi karibuni Aprili 10, Ofisi ya Waziri Mkuu imetangaza katika taarifa.
Licha ya maandamano, serikali ya Israeli imeidhinisha kufutwa kazi kwa Ronen Bar siku ya Ijumaa, Machi 21. Mkuu wa Idara ya usalama wa ndani, Shin Bet, amepoteza imani ya Benjamin Netanyahu.
Barua ya Waziri Mkuu kwa wajumbe wa serikali imetaja “kupotea kwa uaminifu wa kitaaluma na kibinafsi kati ya Waziri Mkuu na Mkurugenzi wa idara,” ambaye anazuia “Serikali na Waziri Mkuu kutumia mamlaka yao ipasavyo, na kudhoofisha uwezo wa kiutendaji wa utumishi na utawala wa nchi.”
“kupoteza imani (…) kumeimarishwa wakati wa vita, zaidi ymbali na kushindwa kwa operesheni ya Oktoba 7, na hasa katika miezi ya hivi karibuni,” barua hiyo inaongeza, ikirejelea mashambulizi ya umwagaji damu ya Hamas kusini mwa Israeli mnamo Oktoba 7, 2023, ambayo yalianzisha vita huko Gaza.
Ronen Bar, aliyeteuliwa Oktoba 2021 kwa muhula wa miaka mitano, alikuwa amehakikisha hata kabla ya uamuzi kwamba atajitetea mbele ya “mamlaka husika”.
Katika barua iliyotangazwa hadharani siku ya Alhamisi jioni, alisema kwamba nia za kufutwa kwake kazi, zilizotangazwa Jumapili na Benjamin Netanyahu, ziliegemea kwenye “maslahi ya kibinafsi” na ililenga “kuzuia uchunguzi wa matukio ya Oktoba 7 na kesi zingine mbaya kuchunguzwa na Shin Bet.”
Tangazo la Jumapili la kuashiria kufutwa kazi kwake lilizua hasira miongoni mwa upinzani na kusababisha maandamano ambayo yalilaani “tishio kwa demokrasia” na kumshutumu Benjamin Netanyahu kwa kutaka kujilimbikizia madaraka.
Siku ya Alhamisi jioni, maelfu kadhaa ya watu walisimama kwenye mvua na upepo kuandamana nje ya makazi ya kibinafsi ya Benjamin Netanyahu huko Jerusalem, na kisha nje ya Knesset, bunge la Israeli, ambapo mawaziri walikuwa wakikutana.
Sababu zisizo za wazi
Ronen Bar alikuwa tayari amedokeza kwamba angejiuzulu kabla ya mwisho wa muda wake, lakini kwa masharti yake mwenyewe na kuhakikisha jukumu la kushindwa kwa idara yake kuzuia shambulio hilo.
Uchunguzi wa ndani wa Shin Bet, uliowekwa hadharani mnamo Machi 4, ilikiri dosari katika mkusanyiko wa kijasusi ambao ungefahamisha mamlaka. Pia aliikosoa serikali, na Benjamin Netanyahu kwa njia isiyo ya moja kwa moja, akisema kwamba sera ya kutuliza vuguvugu la Kiislamu la Palestina katika miaka ya hivi karibuni “imeruhusu Hamas kujenga safu ya kijeshi yenye kuvutia.”
Katika barua yake, iliyowekwa hadharani siku ya Alhamisi jioni, Ronen Bar alisema hoja za Waziri Mkuu ni “tuhuma za jumla, zisizo na uthibitisho (…) ambazo zinaonekana kuficha sababu nyuma ya uamuzi wa kumfuta kazi.”
Anarejelea hasa “uchunguzi tata, wa kina na nyeti sana” unaohusisha watu wa karibu na Benjamin Netanyahu ambao wanadaiwa kupokea kiasi cha pesa kutoka Qatar, jambo lililopewa jina la “Qatargate” na vyombo vya habari.
Kufutwa kazi kwa Ronen Bar kunakuja baada ya jeshi la Israel kuzindua mfululizo wa mashambulizi makubwa na mabaya ya mabomu siku ya Jumanne baada ya miezi miwili ya usitishwaji vita na operesheni za ardhini katika Ukanda wa Gaza.
Benjamin Netanyahu alichukua jukumu la operesheni hizi za kijeshi, ambazo alisema zilikusudiwa kuishinikiza Hamas kuwaachilia mateka 58 ambao bado wanazuiliwa katika eneo hilo.
Katika ukosoaji wa nadra dhidi ya waziri mkuu, Rais wa Israeli Isaac Herzog alielezea wasiwasi wake siku ya Alhamisi kwamba kuanza tena kwa mashambulizi wakati nchi inakabiliwa na mgogoro kunaweza kudhoofisha “ustahimilivu wa kitaifa.”