
Safari za ndege za wahamiaji wa Venezuela kutoka Marekani zitaanza tena Jumamosi, Machi 15, baada ya kusimamishwa na serikali ya Venezuela. Baada ya uamuzi wa Washington wa kusitisha leseni ya uchimbaji wa mafuta ya Venezuela, pigo kubwa kwa nchi hiyo ambayo imekuwa ikiishi chini ya vikwazo vya Marekani kwa miaka kadhaa, Caracas ilijibu kwa kukataa kurejea kwa raia wake wanaochukuliwa na Washington kama wahamiaji haramu.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu wa Caracas, Alice Campaignolle
Habari hizo zimewekwa hadharani jana kwenye mtandao wa kijamii wa X na mshauri maalum wa Donald Trump, Richard Grenell. Mwanadiplomasia huyu, ambaye alikuja kufanya mazungumzo na Nicolas Maduro mwanzoni mwa mwaka huu, alisema “alifurahishwa” na uamuzi huu kutoka kwa Caracas.
Wavenezuela 600,000 washio Marekani kinyume cha sheria
Kiongozi wa upinzani Jesus Torrealba anasema udhalilishaji huu wa wananchi wenzake ni kashfa. “Sikubaliani na madai kwamba watu hawa hawana hadhi ya ukimbizi inayoendana nao kulingana na Umoja wa Mataifa. Lakini jamani… wakifukuzwa ni bora warudi nchini kwao. “Tunashuhudia vitendo vya udhalilishaji, vya aibu kwa wahamiaji wa Venezuela,” analaumu.
Kufikia sasa, zaidi ya Wavenezuela 600, kati ya 600,000 wanaoishi kinyume cha sheria nchini Marekani, wamerudishwa katika nchi yao ya asili tangu mwezi wa Februari, wakati safari za ndege za kuwarejesha nyumbani zimeanza tena kati ya Venezuela na Merikaarekani. Kukataa kwa Caracas kuwapokea wahamiaji wake kwa muda mrefu imekuwa njia ya kutoa shinikizo.
Swali sasa ni je Ikulu ya White House ilimuahidi nini Maduro kubadili mawazo yake? Je, kampuni ya mafuta ya Marekani Chevron itaendelea kufanya kazi nchini Venezuela?