Kocha asiyeona, anavyojipanga kutamba soka la Tanzania

“Watu hawaamini kama nina uwezo wa kufundisha soka kwasababu tu siwezi kuona. Hilo linanipa wakati mgumu japo kama mwalimu wa mpira wa miguu inanipa nafasi ya kujiamini zaidi,” anaeleza Kocha wa timu ya Mfaranyaki City, Priver Ngonyani. BBC ilifika katika uwanja wa Mfaranyaki uliopo wilayani Songea, kusini mwa Tanzania kuzungumza naye.