Dar es Salaam. Licha yawatumiaji wa huduma za kifedha kuendelea kuongezeka nchini, bado huduma nyingi za kifedha zimeendelea kumbebesha mwananchi wa kawaida mzigo wa gharama za huduma.
Watoa huduma wanaotaka kurejesha faida ya uwekezaji wao wamekuwa wakiongeza viwango vya juu vya makato, kuchangia kurudisha nyuma maendeleo ya Watanzania wa kipato cha chini.
Ni Selcom Microfinance Bank Limited pekee ndiyo inayowaza tofauti na watoa huduma wengine kupitia Selcom Pesa. Ikiwa ni huduma ya kifedha mpya mjini iliyozinduliwa hivi karibuni, Selcom Pesa inakwenda kujenga uzoefu mpya kwa Watanzania wa kufanya miamala ya kifedha yenye unafuu zaidi kuwahi kutokea nchini.
Uzinduzi wa Selcom Pesa ni sehemu ya juhudi zinazoendelea za kuhamasisha mageuzi ya kiuchumi na kidigitali nchini, chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom Microfinance Bank Limited, Julius Ruwaichi amefanya mahojiano maalumu na timu ya Gazeti la Mwananchi ofisini kwake. Na hii ni sehemu ya mazungumzo hayo:-

Mteja wa Selcom Pesa anaweza kufanya malipo kwa kadi bure, hakuna makato.
Swali: Selcom Pesa ni nini? Imeanzishwa kwa malengo gani?
Ruwaichi: Selcom Pesa ni huduma mpya ya kifedha inayompa mteja fursa ya kufanya miamala yote ya kibenki kidigitali au kwa kutumia mfumo wa Programu Tumishi (App), ikiwa na Makato Madogo Kuliko benki zote na mitandao yote ya simu. Ukitumia Selcom Pesa unaokoa zaidi ya asilimia 60% ya makato unayoyapitia kwenye benki yako ama mtandao wako wa simu.
Benki yetu inasimamiwa na Benki ya Kuu Tanzania (BoT), kwa hiyo, mtumiaji yeyote wa huduma hii analindwa kisheria na anakuwa anatumia huduma halali ya kibenki.
Swali: Je, hamdhani utozaji wa makato madogo ambayo ni sawa na bure ni mkakati wa kimasoko tu?
Ruwaichi: Benki yetu inajitahidi kuhakikisha kuwa tunakuwa sehemu ya mafanikio ya Watanzania wengi kwa kuwapatia huduma ambayo ni nafuu na zinazoendana na mazingira halisi ya Watanzania wa kipato cha chini.
Huduma za Selcom Pesa zinapitia katika mfumo wa uhamishaji fedha wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ujulikanao kama TIPS ambao hauna gharama kwenye kuhamisha fedha.
Kama tuliona ipo haja ya kuwaletea Watanzania huduma rahisi ya kufanya miamala yao kwa makato madogo kuliko, si busara sana kujipatia faida kwa kutoza gharama kubwa ikiwa sisi hatutozwi gharama kupitia mfumo wa BoT.
Sisi tumemua kuweka makato madogo ili kuwapa Watanzania huduma za kifedha endelevu na himilivu. Na tutaendelea kuwa hivi hivi hata kwa siku zijazo ili kila mtu anufaike na mfumo huu na afikie malengo yake kiuchumi kupitia sisi.
Swali: Kwa nini nitumie Selcom Pesa?
Ruwaichi: Moja ya faida za kutumia Selcom Pesa ni urahisi na unafuu. Mteja anayetumia SelcomPesa anapata unafuu wa gharama za miamala kwa zaidi ya asilimia 60 ukilinganisha na watoa huduma nyingine.
Pia, kama umewahi kutumia huduma yetu, utagundua ni mfumo rahisi na wenye uharaka zaidi. Unaweza kupakua na kujisajili mwenyewe na kuanza kuutumia ndani ya dakika zisizozidi tatu.
Swali: Huduma gani zinapatikana kwenye Selcom Pesa?
Ruwaichi: Kupitia Selcom Pesa, huduma zipatikanazo ni nyingi. Mteja anaweza kutuma fedha kutoka Selcom Pesa kwenda benki yoyote nje na ndani ya nchi, anaweza kutuma kwenda kwenye mtandao wowote wa simu, kufanya malipo ya bili zote za Serikali (umeme, maji, kodi, TRA nk), kulipia bili binafsi (huduma za ving’amuzi, bima, intaneti, usafiri, kubeti, muda wa maongezi, hisa na dhamana) kulipia bidhaa madukani (yenye lipa namba aina zote ikiwemo za benki au mitandao ya simu),
kuweka akiba (kupitia kibubu) nk.
Swali: Utaratibu wa kujiunga na Selcom Pesa ukoje?
Ruwaichi: Kwa mteja mwenye simu janja, atatakiwa kupakua aplikesheni ya Selcom Pesa kutoka kwenye Playstore/ Apple Store na kutakiwa kuwa na namba ya NIDA tu kujisajili mwenyewe.
Ukishafungua App, utajisajili kwa kufuata maelekezo na baadaye kuweka alama za vidole na picha ya sura yake kama uthibitisho wa mtu tunayemuingiza kwenye mfumo wetu ni sahihi. Ni njia rahisi kujiunga na rafiki pia. Sio kila mtu ana simu janja.
Kwa upande wa wateja wanaotumia ’viswaswadu’, wanaweza kutumia USSD namba *150*35# kupata huduma ya Selcom Pesa, lakini hatua ya ya kijisajili ni lazima wafike kwa wakala wa Selcom Pesa au matawi yetu, wataungwanisha na kuweza kupata huduma zote za kifedha. Kwa utaratibu huo, tunaamini tutafikia nchi nzima.
Swali: Kwa kiasi gani mmewekeza katika teknolojia?
Ruwaichi: Tunao mkakati wetu wa kibenki ambao umejikita katika mageuzi ya kidijitali ambao umeweka teknolojia mbele kama dira yetu.
Benki yetu ipo chini ya muwekezaji mwenye uzoefu mkubwa wa teknolojia, aliyepo sokoni kwa zaidi ya miaka ishirini akitoa huduma za kifedha na malipo kidigitali huku Selcom Pesa ikiwa ni zao la jitihada hizo. Teknolojia kwetu ni maisha ya kila siku.
Swali: Je, mteja wa Selcom Pesa anaweza kutumia kadi?
Ruwaichi: Kadi zipo na mteja wa Selcom Pesa atakuwa na fursa ya kutumia za aina mbili; kadi ya plastiki ambayo ni Mastercard unayoweza kutumia kufanya malipo aina zote kupitia POS mashine zote, iwe kwenye mgahawa, vituo vya mafuta au supermarket.
Na Selcom Pesa kadi ya kieletroniki ambayo inakuwezesha kufanya malipo aina yote ya online. Kikubwa ni hakuna gharama za makato unapotumia kadi zetu kufanya miamala, ni BURE kabisa, utalipia tu gharama ya huduma yako, hakuna makato ya ziada.
Swali: Je, kwa kiasi gani ulinzi umezingatiwa?
Ruwaichi: Ni lazima kuwe na ulinzi wa miamala, taarifa na uendeshaji mifumo. Na ndiyo unapojiunga na aplikesheni yetu ya Selcom Pesa, kujisajili nia lazima tupate uthibitisho wa alama za vidole vyako, na uhakiki wa mfumo wa NIDA unao kutambua kitaifa.
Pia, unapoendelea kuitumia aplikesheni yetu ya Selcom Pesa, ni lazima uingie kwa ukaguzi wa sura na namba yako ya siri inahusika kukutambua kabla haijakuruhusu kutumia huduma.
Lakini, tumewekeza pia katika kufundisha watu wa ndani jinsi ya kulinda, kukagua na kuibua hatari za wizi wa mitandaoni. Huduma zetu za masaa 24 zinawapa wateja nafasi ya kuwasiliana nasi endapo atahisi kuna viashiria au mazingira ya utapeli unataka kutokea ili tuweze kuchukua hatua. Mwasiliano yetu ambayo ni namba za bure kabisa ni
0800 714 888 au 0800 784 888.
Swali: Mmejipanga kiasi gani kuhakikisha huduma hii inawafikia Watanzania wote?
Ruwaichi: Kama nilivyoongea pale mwanzoni, tunataka bidhaa hii iende kwa Watanzania wote na jambo zuri tuna matawi zaidi ya 10 nchi nzima, lakini tunayo huduma iitwayo ‘Selcom Huduma’, mtandao wa mawakala wa Selcom waliopo zaidi ya 25,000 nchi nzima, wenye kutoa huduma zote za kifedha na kuunganisha wateja wetu wote.
Kwa kadri muda unavyozidi kwenda, tutaendelea kubuni njia mpya za kuifikisha huduma hii kwa watu wetu.
Swali: Tuelezee kuhusiana na kampeni yenu ya 5 kwa Jero
Ruwaichi: Benki yetu ipo katika kampeni maalumu ya 5 kwa Jero, Bando la Miamala ambayo inaibeba bidhaa yetu ya Selcom Pesa. Hii ni mara ya kwanza hapa nchini ambapo wateja wanapewa kifurushi cha kufanya miamala.
Kampeni ya 5 kwa Jero Bando la miamala, linakuwezesha
kufanya miamala mitano kwa makato y ash. 500 tu, siku nzima, kwa kiwango chochote cha fedha. Muamala wa kwanza wa siku wa tuma kwenda benki, mtandao wa simu au LIPA NAMBA utachajiwa Sh 500, kisha miamala minne inayofuata ni BURE!
Tunapenda kuwasisitizia Watanzania watumie huduma za Selcom Pesa ili kujikomboa kwenye mzigo wa mkubwa wa miamala, makato kausha damu, kwani Selcom Pesa ina Makato Madogo kuliko benki zote na mitandao yote ya simu.
Selcom Pesa inapatikana kwenye mitandao ya kijamii, ikiwemo Facebook, Instagram, X, Linkedin na Tik Tok, kwa jina hili hili @ selcompesa. Pia taarifa zetu zinapatikana kwenye website https://www