Aucho, Mukwala kusaka fainali Kombe la Dunia 2026

KIUNGO wa Yanga, Khalid Aucho na mshambuliaji wa Simba, Steven Mukwala wameitwa katika kikosi cha Uganda kinachojiandaa na mechi mbili za kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2026 zinazotarajiwa kupigwa hivi karibuni.

Kocha wa Uganda, Paul Put ameita kikosi hicho chenye mchanganyiko wa wachezaji wanaocheza katika klabu za Uganda na wale wa timu za nje ya nchi hiyo.

Katika kundi hilo amewajumuisha Aucho na Mukwala ambao walikuwemo kikosini pindi timu hiyo ilipocheza mechi mbili za kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon), zitakazofanyika nchini Morocco.

Timu hiyo itacheza na Msumbiji, Machi 20 ikiwa ugenini na baada ya hapo, Machi 25, watacheza dhidi ya Guinea ilhali baada ya mchezo huo kambi itavunjwa na wachezaji kurejea kwenye klabu zao.

Kocha wa kikosi hicho amewaita wachezaji 26 wakiwamo makipa watatu, mabeki wanane, viungo saba na washambuliaji wanane.

Kikosi cha Uganda kinaundwa na makipa Isima Watenga, Alionzi Nafiani na Mutakubwa Joel, huku mabeki ni Bwomono Elvis (St Mirren FC), Kizito Gavin (KCCA), Mugabi Bevis (Anorthosis Famagusta), Awany Timothy  (Ashdod), Sibbick Toby (Wigan Athletic), Torach Rogers (Vipers), Kayondo Abdu Aziizi (Slovan Liberec) na Muleme Isaac (Viktoria Zizkov).

Viungo ni Ssekiganda Ronald (SC Villa), Semakula Kenneth (Club Africaine), Aucho (Yanga), Ssebagala Enock (NEC FC), Watambala Karim (Vipers), Okello Allan (Vipers) na Mutyaba Travis (Girondins).

Washambuliaji ni Omedi Denis (APR), Kiwanuka Hakim (APR), Ssemugabi Jude (Kitara), Mato Rogers (Vardar), Mukwala (Simba),  Muhammad Shaban (Al Anwar Al Abyar), Kabuye Calvin (Mjallby AIF) na Kakande Patrick (SC Villa).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *