
Wiki tatu baada ya M23 inayoungwa mkono na Rwanda kuchukuwa udhibiti wa mji wa Bukavu, mji mkuu wa Mkoa wa Kivu Kusini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ukosefu wa usalama unatawala mji huo.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Mjini Bukavu, wiki tatu baada ya waasi wa M23, wanaoungwa mkono na Rwanda, kuuteka mji huo, watu wanauawa na nyumba kushambuliwa na majambazi wenye silaha karibu kila jioni. Kulingana na mashahidi, wengi wanaoshukiwa kuwa wahalifu pia huuawa usiku na wakaazi wenye hasira.
Hali hii mbaya ya inatia wasiwasi mashirika ya kiraia, mashirika yanayotetea haki za binadamu. Amos Bisimwa ni mwanaharakati katika vuguvugu la kiraia la Observatory of Parliamentary and Governmental Actions (OBAPG) nchini DRC, anaelezea kuhuzunishwa kwake na antoa wito wa kurejeshwa kwa hali ya usalama: “hakuna siku ambayo inakwenda kombo bila kuripotiwa zaidi ya vifo 12 katika jiji la Bukavu. Angalau kumi na wwawili wamefariki! “
“Watu kujichukulia sheria mkononi”
“Wiki iliyopita,” amesema, “tulirikodi hadi vifo 14 kwa siku. Watu wanaouawa na watu kwanajichukulia sheria mkononi ) lakini pia kwa kulipizana kisase. Kando na wale wanaochomwa moto katika kundi la watu, wengine wengi hupigwa risasi kichwani. “
“Ukosefu wa usalama unasababishwa hasa na wafungwa waliotoroka jela kutoka magereza mbalimbali katika jiji la Bukavu na viunga vykae; Inaweza kukadiriwa kuwa kuna zaidi ya wafungwa 5,000 waliotoroka. Wakitumia fursa ya silaha zilizotelekezwa mitaani na waajeshi wa jeshi la DRC, FARDC, waliokimbia, hizi ndizo silaha wanazotumia kufanya idadi ya watu kukosa usalama na kuua raia wasiokuwa na hatia. Pendekezo ni kwamba haki ianze tena shughuli zake ili kupunguza hali hii, na kwamba maafisa wa polisi waliotumwa Kivu Kaskazini kwa mafunzo ya kulipenda taifa warudi kama jambo la dharura ili kuhakikisha utulivu wa umma,” Amos Bisimwa pia ameeleza.