Dar es Salaam. Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi amesema kuna haja kwa mataifa ya Afrika Mashariki kuanzisha mfuko wa nishati utakaowezesha kugharimia utafiti, maendeleo na ubunifu katika mafuta na gesi.
Amesema hatua hiyo itayawezesha mataifa hayo kukabili-ana na changamoto za kifedha za uendelezaji wa miradi ya nishati zinazosababishwa na mashinikizo ya wanaharakati duniani.
Dk Mwinyi amesisitiza kuwa kumekuwa na wimbi la wanaharakati duniani wanaoshinikiza wafadhili wasitoe fedha kugharimia miradi inayohusisha nishati isiyo safi.
Hata hivyo, kauli hiyo inaakisi kilichowahi kushuhudiwa katika mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania, uliokabiliwa na upinzani kutoka kwa wanahara-kati wa Ufaransa.
Dk Mwinyi amesema hayo leo, Ijumaa, Machi 7, 2025, katika hotuba yake ya kuhitimisha Kongamano na Maonye-sho ya 11 ya Petroli yaliyofanyika kwa siku tatu katika Kit-uo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Amesema hakuna muda mwafaka zaidi ya sasa wa kuhakikisha kunaanzishwa mfuko wa nishati kwa ajili ya kutimiza mikakati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka 2014.
Amesema mfuko huo ni muhimu kwa ajili ya uwezeshaji wa mafunzo, utafiti, maendeleo na ubunifu katika sekta ya ma-futa na gesi.
Dk Mwinyi amesema uhaba wa fedha ni moja ya mambo yaliyobainika kuwa kikwazo cha uendelezaji wa sekta ya mafuta na gesi katika nchi za Afrika Mashariki.
Katika msisitizo wa uwezeshaji wa kifedha, amesema EAC inapaswa kuanzisha mfuko wa nishati kwa ajili ya kukabili changamoto hizo.
“Katika kipindi ambacho wanaharakati duniani wanasisitiza upinzani dhidi ya ufadhili wa miradi ya nishati isiyokubali-ka na kusisitiza wadau wasiwezeshe.
“Ni vema kujiuliza kama nchi wanachama tunawezaje kutatua changamoto hii na hatimaye kuendeleza vyanzo vyetu vya nishati ya mafuta na gesi na kutimiza mipango yetu ya mageuzi ya nishati ipasavyo,” amesema.
Amesema ni muhimu kutambua kuwa teknolojia inakwen-da kwa kasi zaidi hasa katika sekta ya mafuta na gesi.
“Tunashuhudia mbinu rahisi za uziduaji wa nishati hizi, mambo ambayo yanapunguza uzalishaji wa hewa chafu katika viwanda vyetu,” amesema.
Ametaka juhudi za pamoja za kuvuna nishati hizo zitawezesha kugundua maeneo yenye mafuta na gesi katika nchi hizo za kikanda.
Kiongozi huyo amesema kuwa ni muhimu kuelewa kuwa gesi na mafuta ni nishati muhimu katika safari ya mabadili-ko ya matumizi ya nishati.
Pia amesema ni muhimu kuhakikisha katika miradi hiyo, watu wa mataifa husika wananufaika na utekelezwaji wa miradi inayofanyika.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Doto Biteko, amesema mkutano huo ni jukwaa adhimu la kujadiliana kuhusu fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo katika sekta ya mafuta na gesi.
Kutokana na mkutano huo, amesema wamejua namna nchi za Afrika Mashariki zinavyoweza kushirikiana na kutumia rasilimali za nishati ilizonazo kuboresha maisha.
Amesema mkutano huo umehudhuriwa na zaidi ya watu 1,400 kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika Mashariki na kwingineko.
“Mkutano huu umekuwa muhimu kwa kutoa taarifa za fur-sa za uwekezaji zilizopo katika mataifa ya Afrika Mashariki na faida nyingine zilizopo ambazo kila mmoja anaweza kunufaika nazo,” amesema.
Awali, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dk Felchesmi Mramba, amesema kwa siku tatu zote mijadala kuhusu ma-futa na gesi imejadiliwa na mpango wa kuhamia katika nishati jadidifu.
Ameeleza kuwa kulikuwa na fursa za kuwasikiliza wataal-amu kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Wataalamu hao, amesema wameeleza kuhusu hatua iliyof-ikiwa sasa, ijayo na mipango mingine kwa ajili ya kuweke-za kwenye mafuta na gesi.
“Tunapokwenda kuhitimisha mkutano huu, naamini mta-rudi kwenu mkiwa na habari njema kuhusu Dar es Salaam,” amesema.
Akichangia kwenye mjadala huo, Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa Hatari wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Renatus Nyanda, amesisitiza umuhimu wa uwekezaji wa kiuchumi na kuzingatia usimamizi wa athari za mazingira.
“Usimamizi wa mapato yanayotokana na miradi ya mafuta na gesi unapaswa kuzingatia usimamizi wa mazingira na utafiti unaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kufanikisha lengo hilo,” amesema.
Akiwasilisha mada kuhusu ufanisi wa tathmini za athari za mazingira (EIA) katika tafiti za kijiolojia za mafuta nchini, Mtaalamu Mwandamizi wa Jiolojia wa TPDC, Faustin Kayombo, ametoa matokeo ya tafiti zilizofanyika Kil-ombero, Mtwara, na Ruvu.
Amepongeza mchakato wa tathmini za mazingira za Tan-zania, huku akibainisha changamoto, ikiwemo ushawishi wa kisiasa wakati wa utekelezaji wa hatua za kupunguza athari za mazingira.
“Kuna ushawishi wa kisiasa katika utekelezaji wa hatua za kupunguza athari za mazingira.
“Uboreshaji wa utekelezaji na ushirikishwaji wa umma kati-ka mchakato huu ni muhimu,” amesema.
Kuhusu teknolojia bunifu za kulinda mazingira, Ofisa wa Usimamizi wa Mazingira wa GASCO, Nachael Mwanga, ametambulisha suluhisho la kisasa kwa ajili ya kutibu maji taka ya viwandani.
Ameeleza namna teknolojia ya micro na nanobubbles ina-vyoweza kutumika kusafisha maji taka ya viwandani.
“Tunapotumia nanobubbles ndogo badala ya kubwa, tun-aweza kupata matokeo bora zaidi kwa mazingira,” ame-fafanua Mwanga.
Amesisitiza kuwa teknolojia hiyo, isiyotumia kemikali, inaweza kuboresha kwa kiasi kikubwa ubora wa maji na kupunguza athari kwa mazingira.
Katika wasilisho lingine, Mhandisi Mwandamizi wa Petroli kutoka Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini ya Uganda, Winston Mugumya, amezungumzia umuhimu wa uchimbaji wa mafuta kwa uwajibikaji katika maeneo nyeti kimazingira.
“Matumizi ya teknolojia hizi yameleta matokeo chanya, na nahimiza Serikali kutumia teknolojia kama hizi katika mifu-mo yao ya uchimbaji, hasa katika maeneo yenye utajiri wa rasilimali kama Bonde la Ufa,” amesema.