Ayatullah Siddiqi: Chuki dhidi ya Marekani na utawala wa Kizayuni imeenea duniani kote

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema kuwa, adui wa Israel sio kambi ya muqawama tu na kuongeza kuwa, mauaji ya wanawake na watoto huko Gaza na makamanda wa muqawama yamesababisha kusambaa duniani kote chuki dhidi ya utawala wa Kizayuni na Marekani.