Misri yapinga pendekezo la Israel la kutaka Gaza isimamiwe na Cairo

Misri imepinga pendekezo lililotolewa na kiongozi wa upinzani wa Israel, Yair Lapid kwamba Cairo, badala ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas, iendeshe na kuusimamia kwa muda Ukanda wa Gaza; na kusisitiza kuwa mipango ya aina hiyo “haikubaliki.”