EAC na SADC zawateua marais wastaafu wa Afrika kusuluhisha mzozo wa Kongo DR

Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, SADC zimewateua Uhuru Kenyatta kutoka Kenya, Olusegun Obasanjo kutoka Nigeria, na Hailemariam Desalegn kutoka Ethiopia kuongoza mazungumzo ya kutatua mzozo wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).