Kiongozi Muadhamu:  Vitisho vya adui dhidi ya nchi na wananchi wetu havijawa na natija

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, amesema kwamba maandamano makubwa ya watu wetu ya Bahman 22 ya maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu yalithibitisha kwamba vitisho vya maadui dhidi ya nchi yetu na watu wetu havijazaa matunda.