#HABARI: Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limetoa ufafanuzi wa taarifa inayosambaa katika mitandoa ya kijamii kuhusu kutoweka kwa kijana Shadrack Chaula [24] Mkazi wa Kijiji cha Ntokela Wilayani Rungwe mkoani Mbeya ambaye alichoma picha ya Rais huku akitamka maneno ya kumkashifu.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limepokea taarifa za kutoweka nyumbani kwao kijana huyo Agosti 02, 2024 majira ya saa 8:30 mchana kutoka kwa baba mzazi wa kijana huyo aitwaye Yusuph Chaula [56] Mkazi wa Ntokela na limeanza kufanya ufuatiliaji na uchunguzi kuhusu taarifa hizo, hivyo linawataka wananchi kuwa watulivu katika kipindi hiki linapoendelea na uchunguzi.