Imam Khamenei: Wairani wamepuuza vitisho vya kijinga vya adui na kutuma ‘ujumbe wa umoja’ kwenye maadhimisho ya Bahman 22

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amelipongeza taifa la Iran kwa kufikisha “ujumbe wa umoja” kwa jamii ya kimataifa katika maadhimisho ya miaka 46 ya Ushindi wa Mapinduzi ya Kihistoria ya Kiislamu ya Iran ya mwaka 1979.